Home Habari za michezo ZILIZOFUNGWA NA SIMBA KWA MKAPA ..ZOTEE ZAKUTANA FAINAL SHIRIKISHO AFRIKA…SIMBA WALIKOSEA WAPI…?

ZILIZOFUNGWA NA SIMBA KWA MKAPA ..ZOTEE ZAKUTANA FAINAL SHIRIKISHO AFRIKA…SIMBA WALIKOSEA WAPI…?


Klabu ya RS Berkane kutoka nchini Morocco imefanikiwa kutinga hatua ya Fainali Komnbe la Shirikisho Afrika baada ya Kuichapa TP Mazembe kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo jumla ya magoli 4-1.

Ushindi huo wa Berkane unawafanya Wamorocco hao kutinga Fainali kwa jumla ya ushindi wa magoli 4-2 baada ya kukubali kichapo cha goli 1-0 katika mcheo wa kwanza uliopigwa

Katika mchezo huo Mazembe walimaliza pungufu baada ya mchezaji wao wa Kimataifa wa Zambia Tandi Mwape kuoneshwa kadi nyekundu dakika ya 64.

Magoli ya RS Berkane yaliwekwa wavuni na Bakr El Helali, Najji Larbi na Youssef El Fahli aliefunga mabao mawili.

Goli pekee la Mazembe lilifungwa na Phillippe Kinzumbi akisawazisha muda mcheze baada ya kutanguliwa.

Kwa ushindi huo Berkane wanakwenda kukutana na Orlando Pirates Kutoka nchini Afrika ya Kusini katika Fainali ya Kombe la Shirikisho Mei 20, katika Uwanja wa Godswill Akpabio nchini Nigeria.

Berkane wameshatinga Fainali mbili za Shirikisho kwa miaka ya hivi karibuni ambayo ni 2019 wakapoteza kisha wakanyakua ubingwa mwaka uliofuata 2020.

Orlando wametinga Finali baada ya kuiondosha Al – Ahly Tripoli kwa ushindi wa Jumla wa mabao 2-1.

Ajabu ni kwamba timu zote hizo mbili, zilifungwa na Simba SC katika mechi za hapa Tanzania, je unafikiri Simba kuna mahali walikosea au ni kushindwa kujipanga vyema..?

SOMA NA HII  KUTOKA MALAWI: 'VIBE' LA MASHABIKI SIMBA LAITIKISA LILONGWE...WAMALAWI WABAKI KUSHANGAA ...HAWAELEWI KITU AISEE...

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here