Home Habari za michezo IMEFICHUKA….SIMBA KUPINDUA MEZA KIBABE KWA AZIZ KI…MWENYEWE AOMBA KUSAJILIWA MSIMBAZI…

IMEFICHUKA….SIMBA KUPINDUA MEZA KIBABE KWA AZIZ KI…MWENYEWE AOMBA KUSAJILIWA MSIMBAZI…


JINA la Stephen Aziz Ki, kiungo wa ASEC Mimosas, bado linatembea mitaa ya Kariakoo jijini Dar baada ya timu kongwe za hapa nchini, Simba na Yanga kuiwania saini yake.

Winga huyo ambaye hivi karibuni ilielezwa kwamba Yanga wanakaribia kupata saini yake kwa ajili ya msimu ujao, kwa sasa Simba wanaonekana kuwa karibu zaidi kumchukua.

Mchezaji huyo raia wa Burkina Faso, anasimamiwa na mfanyabiashara Idriss Diallo ambaye kwa sasa ni Rais wa Shirikisho la Soka Ivory Coast (FIF).

Chanzo chetu kutoka Simba, kimesema kuwa, baada ya uongozi wa klabu hiyo kuanza harakati za kuiwania saini ya Aziz Ki, ulirudi nyuma kutokana na RS Berkane ya Morocco kuingilia dili hilo.

Mtoa taarifa huyo aliendelea kueleza kwamba, kwa sasa matumaini ya kumpata yamerudi tena baada ya mchezaji mwenyewe kuonesha nia ya kujiunga na Simba, huku akiwapa mbinu za kumpata kirahisi.

“Ilifikia kidogo tu tukate tamaa ya kumnasa Aziz Ki, ila tunamshukuru sana yeye mwenyewe baada ya kuonesha nia ya kutaka kujiunga na sisi.

“Hii ni baada ya kutuambia mtu pekee anayeweza kupokea ofa yetu ni Rais wa Shirikisho la Soka Ivory Coast, Idriss Diallo anayemsimamia ambaye tayari tumemfikia.

“Kitendo cha mchezaji mwenyewe kuonesha nia ya kutaka kuichezea Simba, ndiyo imekuwa chachu yetu kurudi kwa kasi kuhakikisha dili hili linatimia haraka kabla ya mambo kuwa mengi,” kilisema chanzo hicho.

SOMA NA HII  BAADA YA YANGA KUUWASHA MOTO JANA...INJINI HERSI ATO TAMBO ZA KIBABE KWA SIMBA ...

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here