Home Habari za michezo LIGI KUU SIO KITOTO TENA SIMBA,YANGA JUMAMOSI HII

LIGI KUU SIO KITOTO TENA SIMBA,YANGA JUMAMOSI HII

Baada ya kukamilisha majukumu yao ya Kimataifa kwa ushindi mnono, wawakilishi wa nchi katika mashindano ya Klabu Bingwa, Simba SC na Yanga SC, wanarejea kwenye Ligi Kuu ya NBC Jumamosi, Desemba 23, 2023.

Simba ambao walitoka kuwanyoa Wydad Casablanca, wao watakuwa wageni kwa KMC majira ya saa 10:00 jioni huku Yanga waliotoka kuwakaza Medeama watakuwa wageni kwa Tabora United saa 1:00 usiku.

Kwenye msimamo wa Ligi Kuu, Simba wako nafasi ya tatu wakiwa na alama 22, Yanga wapo nafasi ya pili wakiwa na alama 25.

Ikumbukwe, Yanga amecheza michezo 10, Simba amecheza tisa.

SOMA NA HII  NA NYIE NJOONI....SHOO YA HESHIMA