Home Uncategorized HASIRA ZA KADI NYEKUNDU YA BOBAN, MABAO 8 YA SIMBA KWA SINGIDA...

HASIRA ZA KADI NYEKUNDU YA BOBAN, MABAO 8 YA SIMBA KWA SINGIDA UNITED ZIMEISHIA KWA MBEYA CITY


BAADA ya kupewa zigo la mabao na Simba Uwanja wa Taifa wa mabao 8-0 huku nyota wao Haruna Moshi ‘Boban’ akiambulia kadi nyekundu, leo Singida United wamemaliza hasira zao kwa kuichapa Mbeya City mabao 2-1.

Mchezo huo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa Uwanja wa Namfua ulikuwa na ushindani mkubwa kwa timu zote kusaka pointi tatu muhimu.

Mbeya City ilianza kuitungua Singida United dk ya 15 kupitia kwa Mohamed Kapeta ambapo lilisawazishwa na Erick Mambo dk ya 71 na lile la pointi tatu likifungwa na Elinywea Sumbi dk ya 81.

 Huu unakuwa ushindi wa tatu kwa Singida United inayohaha kujinasua kutoka nafasi ya 20 ikiwa imecheza mechi 29 na ina pointi 15.

SOMA NA HII  RATIBA YA LIGI KUU BARA LEO OKTOBA 22, YANGA NA SIMBA KAZINI