Home Uncategorized KUMEKUCHA JANGWANI, HAWA HAPA PANGA LINAWAHUSU JUMLAJUMLA

KUMEKUCHA JANGWANI, HAWA HAPA PANGA LINAWAHUSU JUMLAJUMLA

ERICK Kabamba, Yikpe Gnamien,David Molinga, ni miongoni mwa wachezaji wa kigeni ambao wanajadiliwa na uongozi wa Yanga ili kujua hatma yao ndani ya kikosi hicho ambacho kinaelekea kufanya mabadiliko makubwa.

Habari zinaeleza kuwa licha ya Molinga kuwa mfungaji namba moja wa kikosi hicho bado, Kocha Mkuu Luc Eymael hajaelewa mchango wake akiwa uwanjani jambo linalompasua kichwa.

“Kuna wachezaji ambao wataondoka baada ya msimu wa Ligi Kuu Bara kuisha kinachosubiriwa ni ripoti kutoka kwa kocha atakachokisema ndicho kitafanyika lakini kwanza tuwatazame kwa muda huu,” kilieleza chanzo hicho.

Yanga ikiwa imecheza mechi 26 imefunga mabao 30 na kinara wa kutupia ni Molinga mwenye mabao 8 akifuatiwa na Patric Sibomana mwenye mabao matano.

SOMA NA HII  NYOTA PULISIC ALICHUNIWA SIKU TATU MAZIMA