Home Uncategorized NYOTA PULISIC ALICHUNIWA SIKU TATU MAZIMA

NYOTA PULISIC ALICHUNIWA SIKU TATU MAZIMA


CRISTIAN Pulisic, mwenye miaka 21 anayekipiga ndani ya Klabu ya Chelsea amesema kuwa siku ya kwanza wachezaji wenzake walimchunia ndani ya gari.

Nyota huyo alijiunga Chelsea akitokea ndani ya Borussia Dortmund kwenye usajili wa majira ya joto anavaa jezi namba 22.

Mshambuliaji huyo amesema siku ya kwanza alipanda basi la timu ya Chelsea kwenda mazoezini hakuna aliyemfahamu wala kumsemesha.

Ameongeza kuwa hakuna ambaye alimtakia kila la kheri kwenye maisha yake mapya jambo lililomfanya ajiulize mara mbili yupo sehemu gani.


 “Siku tatu za mwanzo hakuna mchezaji aliyekuwa akinijali kila mtu aliniona ni mtu wa kawaida ila nilipoanza kufunga na kutoa pasi za mabao wakaanza kunipa ushirikiano,” amesema.

SOMA NA HII  RASTA STARS ANAYEWINDWA NA YANGA AKUBALI KUSAINI SIMBA