Home Uncategorized SOLSKJAER: SARE NI KIPIMO CHA UWEZO WA WACHEZAJI WANGU

SOLSKJAER: SARE NI KIPIMO CHA UWEZO WA WACHEZAJI WANGU


OLE Gunner Solskjaer,  Kocha Mkuu wa Manchester United amesema kuwa sare waliyopata jana kwa kufungana mabao 2-2 dhidi ya Southampton kwenye mchezo wa Ligi Kuu England ni kipimo kwa wachezaji wake kujua uwezo wao.

Mchezo huo ulikuwa  na ushindani mkubwa ambapo United walikuwa wanahitaji pointi tatu ili watinge jumla nne bora huku Southampton wakisaka pointi tatu wajiandalie mazingira ya kuingia 10 bora.

Mabao ya Southampton kwenye mchezo huo uliochezwa Uwanja wa Old Trafford yalifungwa na Armstrong dakika ya 12 na Obafemi aliyeua ndoto ya United kutinga top 4.

Yale ya United yalifungwa na Rashford dakika ya 20 na Martial dakika ya 23 na kuwafanya wagawane pointi mojamoja huku United ikibaki nafasi ya tano ikiwa na jumla ya pointi 59 baada ya kucheza mechi 35.

“Wakati mwingine unawapa kazi vijana wako kisha unaangalia uwezo wao pamoja na namna ambavyo wanajituma, kushindwa kufikia malengo sio mwisho wa ushindani, ” amesema.

SOMA NA HII  SIMBA HALI SI SHWARI LIGI KUU...... NAMUNGO WAFANYA UKATILI WA KULAZIMISHANA