Home Uncategorized HAWA HAPA NDANI YA LIGI KUU BARA NI MWENDO WA 41 KIBINDONI...

HAWA HAPA NDANI YA LIGI KUU BARA NI MWENDO WA 41 KIBINDONI POINTI


MECHI 36 ambazo wamecheza ndani ya dakika 3,240 ngoma imeleta pacha matata kwa upande wa pointi kibindoni na wameogeza Vita ya timu kushuka Daraja.

Timu nne kibindoni zina jumla ya pointi 41 zote zimebakiwa na mechi mbili mkononi.

Mtibwa Sugar ina pointi 41 ipo nafasi ya 14 imeshinda mechi 10, sare 11 imepoteza 15 na safu ya ushambuliaji imefunga mabao 27 huku ikifungwa mabao 32.

Lipuli ipo nafasi ya 15 imeshinda mechi 11 sare 8,poteza 17 safu ya ushambuliaji imefunga mabao 42 na imefungwa mabao 44.

Mwadui FC nafasi ya 15 imeshinda 10, sare 11 poteza 15 imefunga mabao 31 na kufungwa 44.

Alliance nafasi ya 17, imefungwa 15 imeshinda 10 sare 11 na imefungwa mabao 44 huku wakifunga mabao 26.


Zote zimebakiwa na mechi mbili mkononi hivyo ili ziongeze uhakika wa kubaki ndani ya ligi lazima zishinde mechi zote zilizobaki kwenye timu hizo.

Kisha ikiwa wataendelea kugongana pointi itatazamwa idadi ya mabao ya kufunga na kufungwa kumpata mshindi.

SOMA NA HII  SIMBA YASHINDA MABAO 3-1 MBELE YA CHIPUKIZI