Home Habari za michezo MGOSI AFUNGUKA A-Z NAMNA ANAVYOIPIGANIA SIMBA SC NYUMA YA PAZIA…

MGOSI AFUNGUKA A-Z NAMNA ANAVYOIPIGANIA SIMBA SC NYUMA YA PAZIA…

Habari za Simba

Kocha msaidizi wa Simba SC, Mussa Hassan ‘Mgosi’ amesema kutokana na kujua machungu na raha wanazopitia wachezaji, timu ikifanya vizuri ama vibaya, anajua namna ya kuwarejesha kwenye mstari.

Nahodha huyo wa zamani wa timu hiyo, ambaye kwa sasa ni msaidizi wa Kocha mkuu, Juma Mgunda alisema wachezaji ni binadamu na wanapitia changamoto nje ya soka, hivyo wanatakiwa kujengwa kiakili warudishe kujiamini katika majukumu yao.

“Nimepitia huko. Naelewa nikimwona mwingine anapitia huko. Najua kuna nyakati za furaha na changamoto za kupanda na kushuka kiwango.”

“Uzuri kocha mkuu Juma Mgunda kacheza, anaelewa jinsi ya kuwasaidia ili kila mmoja atimize majukumu yake, Seleman Matola pia kacheza anaelewa, naamini wachezaji walifaidi vitu vingi kutoka kwake.”

Mgosi alisema pia mchezaji anapaswa kutumia vyema fursa za uwepo wake Simba SC, kuhakikisha anaacha rekodi zitakazompa heshima akistaafu.

“Ipo mifano mingi ya wachezaji wa zamani wanaotajwa hadi sasa kwenye kikosi hiki ni kwa sababu ya kazi zao, hilo pia lazima walijue litafanya wapambane ili kujiwekea heshima zao za baadaye,” alisema.

Wakati huo huo, Meneja wa Mtibwa Sugar, Henry Joseph amewashauri wachezaji wa kikosi hicho, akiwakingia kifua kuna nyakati wanakuwa na nyakati ngumu zinazohitaji kuwatia moyo.

“Ukiachana na kuwaona wachezaji uwanjani, nyuma ya pazia wana familia zao, hivyo wanaweza wakawa wanapitia changamoto nyingi, ni rahisi kukaa nao chini ili wasitoke kwenye mstari wa majukumu yao,” alisema.

SOMA NA HII  BAADA YA KUANZA KWA KASI YANGA...NKANE AKUTWA NA GONJWA LA AJABU..KUKAA NNJE MPAKA....