Home Uncategorized MZUNGU WA YANGA KUKUTANA NA KIGINGI HIKI NDANI YA LIGI KUU BARA

MZUNGU WA YANGA KUKUTANA NA KIGINGI HIKI NDANI YA LIGI KUU BARA


KOCHA wa Yanga, Luc Eymael anakibarua kizito cha kumenyana na Coastal Union, Februari 23 kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara utakaochezwa Uwanja wa Mkwakwani.

Eymael amekiongoza kikosi chake kupata sare tatu mfululizo, ilianza mbele ya Mbeya City kwa kufungana bao 1-1 kisha ikifauata Tanzania Prisons ya bila kufungana zote Uwanja wa Taifa na ikalazimisha sare ya kufungana bao 1-1 mbele ya Polisi Tanzania Uwanja wa Ushirika, Moshi.

Atakutana na Coastal Union iliyo chini ya Juma Mgunda ambayo imetoka kupapaswa mabao 2-1 na Ruvu Shooting.

Mchezo wa kwanza uliochezwa Uwanja wa Uhuru, Coastal Union iliacha pointi tatu Dar kwa kufungwa bao 1-0.

Charles Mkwasa, Kocha Msaidizi wa Yanga amesema kuwa wanawaheshimu wapinzani wao watapambana kupata matokeo mazuri.

SOMA NA HII  VIDEO: TUNDU LISU AVULIWA UBUNGE