Home Uncategorized MASAU BWIRE HANA DOGO AWAPIGA MKWARA HUU POLISI TANZANIA

MASAU BWIRE HANA DOGO AWAPIGA MKWARA HUU POLISI TANZANIA


OFISA Habari wa Ruvu Shooting, Masau Bwire amesema kuwa wamejipanga kuacha alama nzuri kwa Polisi Tanzania itakayowafanya waikumbuke timu yao msimu mzima kwa kuchukua pointi tatu zao.

Ruvu Shooting itamenyana na Polisi Tanzania, Jumamosi, Uwanja wa Ushirika Moshi kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara.

“Tumeweka kampeni maalumu ya kuondoka na pointi tatu kwenye kanda hii ambayo tupo kwa sasa, tumemalizana na Coastal Union sasa ni zamu ya Polisi Tanzania tutaacha alama ambayo itawafanya wapinzani wetu watukumbuke.

“Timu inapiga mpira wa darasani kama ulaya, pasi nyingi utadhani Barcelona ila kikubwa ni pointi tatu tunatafuta,” amesema.

SOMA NA HII  LIPULI:NJOONI SAMORA MPATE BURUDANI