Home Uncategorized SIMBA YAINGIA KWENYE MTIHANI MZITO WA BIASHARA BONGO

SIMBA YAINGIA KWENYE MTIHANI MZITO WA BIASHARA BONGO


BAADA ya Simba kuibuka na pointi sita jumla mbele ya Kagera Sugar hesabu zao kwa sasa ni mbele ya Biashara United ya Mara.

Simba ilishinda nje ndani kwa Kagera Sugar, kwenye mchezo wa kwanza uliochezwa Uwanja wa Kaitaba Simba ilishinda mabao 3-0 na mchezo uliochezwa Uwanja wa Taifa, Simba ilishinda kwa bao 1-0.

Ushindi huo umeipa pointi sita Simba mbele ya Kagera Sugar na imewafunga jumla ya mabao manne ndani ya msimu wa 2019/20.

 Februari 22 itakuwa na kazi mbele ya Biashara United kwenye mchezo utakaochezwa Uwanja wa Taifa.

Mchezo wa kwanza Simba ilishinda kwa mabaoa 2-0 na kuwafanya wasepe na pointi tatu jumla, mchezo huo ulimuibua kwa mara ya kwanza kinara wa pasi za mwisho msimu uliopita Ibrahim Ajibu kutoa pasi yake ya kwanza ya bao lililofungwa na Miraj Athuman.

Sven Vandenbroeck, Kocha Mkuu wa Simba amesema kuwa maandalizi yao ni kwa ajili ya mechi zote zinazowahusu na kazi ya wachezaji ni kutoa burudani na kutafuta matokeo.

SOMA NA HII  SIMBA:HAKUNA KOMBE GUMU KAMA SHIRIKISHO