Home Habari za michezo TAKWIMU ZINAONGEA…KWA MZUKA HUU WA SAIDO …SIMBA SC WANAWEZA KUPATA ‘KISUKARI’…

TAKWIMU ZINAONGEA…KWA MZUKA HUU WA SAIDO …SIMBA SC WANAWEZA KUPATA ‘KISUKARI’…

Habari za Simba

SAIDO Ntibazonkiza ameonyesha kwamba anaweza kuwa msaada kwenye kikosi cha Simba SC kufuatia kutupia mabao matatu ‘hat trick’ kwenye mchezo wake wa kwanza wa ligi akiwa na timu hiyo dhidi ya Tanzania Prisons.

Ni kama mashabiki wa Simba SC walisahau kutokuwepo kwa mshambuliaji wao hatari, Moses Phiri ambaye ni majeruhi kutokana na kiwango cha nyota huyo aliyesajiliwa dirisha hili kutoka kwa wachimba madini wa Geita Gold.

Ntibazonkiza alitupia mabao matatu kwenye mchezo huo huku akitoa asisti moja kwenye ushindi wa mabao 7-1 ambao Simba SC imeupata dhidi ya Prisons na kufikisha jumla ya pointi 44.

Hizi ni dondoo muhimu za mchezo huo mabao Prisons ilimaliza pungufu kufuatia kwa Samson Mbangula kuonyeshwa kadi nyekundu kwa kumchezea vibaya Hennock Inonga.

Ntibazonkiza amekuwa mchezaji wa kwanza mpya msimu huu kufunga mabao matatu na kutoa asisti kwenye mchezo wake wa kwanza kwenye ligi.

Hii ni mara ya kwanza msimu huu kufungwa hat trick mbili kwenye mchezo mmoja, mbali na Ntibazonkiza, John Bocco naye aliweka kambani mabao matatu kwenye nyavu za Prisons.

Ndani ya dakika 45 za kipindi cha kwanza Simba SC ilipiga mashuti matano yaliyolenga lango huku Prisons ikipiga mawili.

Idadi ya mabao manane kufungwa kwenye mchezo mmoja ni idadi kubwa zaidi kushuhudiwa msimu huu.

Hiki ni kipigo kikubwa zaidi kwa Tanzania Prisons ambacho imekumbana nacho msimu huu wa 2022/23.

Ushindi huo umeifanya Simba SC kupunguza tofauti ya pointi baina yao na Yanga mabao wapo nyuma mchezo mmoja kutoka tano hadi mbili.

Simb SCA imekuwa timu ya kwanza msimu huu kufunga mabao sita kwenye kipindi cha pili, huku ikiweka rekodi pia kwa kuwa timu ya kwanza kufikisha ‘hat trick’Β  nneΒ  ndani ya msimu mmoja.

Kati ya hizo nne, mbili ni za John Bocco, na nyingine ni Moses Phiri pamoja naye Saido Ntibzonkiza.

Kwa matokeo hayo ya jan Simba SC inafikisha alama 44, katika nafasi ya pili huku ikicheza michezo 19 nyuma ya Yanga SC ambao wako nafasi ya kwanza wakiwa na alama 47 wakicheza michezo 18.

SOMA NA HII  TAIFA STARS YAPOTEZA KWA MKAPA MBELE YA BENIN