Home Habari za michezo WAKATI AKIHAHA HUKU NA KULE…FIFA WAMPA TABASAMU AUSSEMS…..

WAKATI AKIHAHA HUKU NA KULE…FIFA WAMPA TABASAMU AUSSEMS…..

Habari za Michezo

KOCHA wa AFC Leopards, Patrick Aussems, amefurahishwa na urejeo wa wachezaji wake watano kwenye kikosi chake kutokana na kushindwa kuitumikia timu hiyo kufuatia kibano cha Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA).

Wachezaji 10 wa Ingwe hawajacheza mechi tatu za ufunguzi Ligi Kuu Kenya msimu huu wakisubiri maamuzi ya FIFA.

“Urejeo wa wachezaji hawa unaleta morale kwenye timu. Baadhi yao ni wazoefu na nina imani sasa tutanza kuandikisha matokeo mazuri. Ifikiapo Januari wachezaji wote watakuwa wamerejea kikosini tayari kupambana,” alisema Aussems kabla ya mchezo wao wa jana FKFPL dhidi ya Kakamega Homeboyz.

“Ningependa pia kushukuru manejmenti ya timu ambayo imehakikisha kuwa mambo yamekuwa sawasawa kwenye timu.”

Wachezaji 10 ambao bado hawakujumuishwa ni pamoja na wale waliosajiliwa wakati wa dirisha la katikati la msimu wa 2021/22 na wengine waliopandishwa kutoka timu ya vijana ni Emmanuel Lwanga, Ronald Sichenje, Loren James, Victor Otieno, Aboubakar Musha, Nester Olum, Cliff Nyakeya, Josephat Lopaga, Victor Omune na Musa Oundo.

SOMA NA HII  AISEEE!! HII SASA KUFURU...JINA LA PELE LAWEKWA KWENYE KAMUSI