Home Simba SC SIMBA WATUA DR CONGO KAMILI KUIVAA AS VITA

SIMBA WATUA DR CONGO KAMILI KUIVAA AS VITA


WAWAKILISHI wa Tanzania kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika, Simba leo Februari 10 wamewasili salama Kinshasha, DR Congo kwa ajili ya maandalizi ya mwisho ya mchezo wao dhidi ya AS Vita.

Simba chini ya Kocha Mkuu, Didier Gomes ilianza safari jana, Februari 9 kwa kutoka Dar na kuweka kambi ya muda Addis Ababa na leo asubuhi walianza safari kuwafuata wapinzani wao.

Mchezo huo wa kwanza kwa Simba iliyo kundi A unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa kwa timu zote kwa kuwa zinatambuana vema hasa baada ya kuwahi kukutana mara mbili msimu wa 2018.

 Mchezo wa kwanza ambao ulichezwa Congo, Simba ilifungwa mabao 5-0 na AS Vita walipokuja Uwanja wa Mkapa walipoteza kwa kufungwa mabao 2-1 na Simba iliweza kutinga hatua ya robo fainali.

Gomes amesema kuwa wanakwenda wakiwa na kazi ya kusaka ushindi kwenye mchezo huo hivo wanaamini watafanya vizuri ndani ya dakika 90.

“Tunahitaji kuona tunafanya vizuri mchezo wetu wa kimataifa, tutapambana ili kupata matokeo na hilo linawezekana,” .

Nyota Jonas Mkude ambaye alikuwa nje ya uwanja kwa muda kutokana na utovu wa nidhamu naye ni miongoni mwa wachezaji ambao wapo kwenye msafara huo.

SOMA NA HII  KOCHA SIMBA 'AMPIGIA UPATU' MBRAZILI MWENZAKE ASAJILIWE SIMBA...NI YULE GOLIKIPA...