Home Habari za michezo BENCHIKHA AFUNGUKA WALIKIPATA BAADA YA KIPIGO KUTOKA KWA WYDAD

BENCHIKHA AFUNGUKA WALIKIPATA BAADA YA KIPIGO KUTOKA KWA WYDAD

Habari za Simba

Kocha mkuu wa kikosi cha Simba Abdelhak Benchikah amesema kile walichokipata katika mchezo wa juzi dhidi ya Wydad AC kitawafanya wajiandae vyema kuelekea mchezo ujao wa marudiano.

“Yote yaliyotokea hapa yatakwenda kutupa usahihi wa maandalizi mazuri ya mchezo ujao. Eneo tulilokuwa bora tutakwenda kuongeza ili kuimarika zaidi na kwenye mapungufu tutakwenda kuparekebisha.”

Simba itakutana na Wydad AC tena December 19 katika uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar Es Salaam.

Simba inahitaji alama 3 muhimu katika mchezo huo ili ifufue matumaini ya kufuzu hatua ya robo fainali ya Ligi ya mabingwa Afrika.

SOMA NA HII  SIMBA SC KUSHUSHA WACHEZAJI HAWA SITA NA KUKAMILISHA USAJILI WAKE MSIMU HUU