Home kimataifa AISEEE!! HII SASA KUFURU…JINA LA PELE LAWEKWA KWENYE KAMUSI

AISEEE!! HII SASA KUFURU…JINA LA PELE LAWEKWA KWENYE KAMUSI

AISEEE!! HII SASA KUFURU...JINA LA PELE LAWEKWA KWENYE KAMUSI

Pelé, ambalo ni jina la utani la gwiji wa soka marehemu Edson Arantes do Nascimento, limeingizwa rasmi kwenye kamusi likimaanisha kitu ama jambo la “kipekee, kisicholinganishwa”.

Kamusi ya Michaelis ya lugha ya Kireno, ni moja ya kamusi maarufu zaidi nchini Brazili, iliongeza “pele” kama kivumishi kipya.

Kuingizwa kwa jina lake kwenye kamusi kulikuja baada ya kampeni ya Pelé Foundation ya kumuenzi nyota huyo wa kandanda kukusanya saini zaidi ya 125,000.

Pele alifariki mnamo Disemba akiwa na umri wa miaka 82. Gwiji huyo pekee aliyeshinda Kombe la Dunia mara tatu, anachukuliwa kuwa mwanasoka bora zaidi kuwahi kutokea duniani, katika historia.

Wakati wa uchezaji wake wa miongo miwili, alifunga mabao 1,281 akiwa na klabu ya Santos ya Brazil, timu ya taifa ya Brazil na New York Cosmos.

SOMA NA HII  PAMOJA NA KUWA NA KESI YA KUJIBU DHIDI YA KARIA....MANARA AIBUKA NA MAMBO YA SLOGAN...ATAKA SERIKALI IINGILIE KATI..