Home Habari za michezo UCHAGUZI MKUU SIMBA: MANGUNGU ABADILI UPEPO …KALUWA APIGIWA YOWE UKUMBI MZIMA…

UCHAGUZI MKUU SIMBA: MANGUNGU ABADILI UPEPO …KALUWA APIGIWA YOWE UKUMBI MZIMA…

Mkutano Mkuu Simba Leo

Maswali matatu aliyoulizwa Murtaza Mangungu ni kama yamebadili upepo wa zomea zomea kwa baadhi ya wanachama wa klabu ya Simba kwenye uchaguzi mkuu huku mpinzani wake, Moses Kaluwa akishangiliwa kwa nguvu wakati akijinadi.

Mangungu na Kaluwa wanachuana kuwania nafasi ya mwenyekiti wa klabu hiyo kwenye uchaguzi mkuu unaoendelea kwenye ukumbi wa mikutano wa Mwalimu Nyerere, jijini Dar es Salaam.

Mangungu ndiye alifungua dimba kwa dakika tano, wakati akianza kujinadi baadhi ya wanachama ukumbi hapo walikuwa wakizomea, lakini kipindi cha maswali na majibu kilibadili upepo wa zomea zomea hiyo na kuwa watulivu kusikiliza majibu ya mgombea huyo anayetetea kiti chake.

Mangungu aliulizwa maswali matatu na wakati akiendelea kuyajibu wanachama walikuwa watulivu wakimsikiliza kwa makini na alipomaliza baadhi ya wanachama walimshangilia na kusema amepata kura.

Alipoitwa Kaluwa, ukumbi ulilipuka kwa shangwe na moja ya sera zake akiomba kura ni kurudisha nguvu ya matawi ambayo alidai imetoweka.

Sera hiyo iliibua shangwe wakati akiendelea kujinadi huku kwenye maswali, ukumbi uliibua zomea zomea kwa mmoja wa wanachama aliyetaka kufahamu kama ametofautiana na wengine.

“Kelele za kupinga swali hilo zilitawala ukumbini, wengi wa wanachama wakidai sio swali.

Swali lingine ambalo mgombea huyo aliulizwa ni miaka miwili mfululizo Simba haijamfunga Yanga, yeye akipewa ridhaa ya kuwa mwenyekiti wa klabu ataweza kuondoa hilo?. Huku mwanachama mwingine akimuuliza kuhusu kuijua falsafa ya Simba na kuonekana kuwa na kauli za kibinafsi, swali ambalo lilipingwa pia wanachama wengine wakizomea kuwa hilo si swali.

SOMA NA HII  SIMBA YATAJA KILICHOWAPONZA MBELE YA YANGA