Home Habari za michezo MKUTANO MKUU WA SIMBA: MANGUNGU AJIPIGIA ‘UPATU’ KIAINA….AFUNGUKA ISHU YA PROPAGANDA…

MKUTANO MKUU WA SIMBA: MANGUNGU AJIPIGIA ‘UPATU’ KIAINA….AFUNGUKA ISHU YA PROPAGANDA…

Mkutano Mkuu wa Simba Leo

Mwenyekiti wa klabu ya Simba, anayemaliza muda wake, Murtaza Mangungu amesema klabu hiyo iko imara na kuwataka wana Simba kutosikiliza propaganda nyingine.

Mangungu ambaye muda mfupi ujao atakuwa na kibarua cha kutetea kiti chake kwenye uchaguzi mkuu akipewa upinzani na Moses Kaluwa anasema wanasimba wako imara, wanaelewa na wanajua timu yao nini inafanya na zaidi wanahitaji mafanikio.

“Tusisikilize propaganda nyingine kuhusu klabu yetu,” anasema Mangungu alipohutubia mkutano mkuu wa kawaida wa klabu hiyo wenye ajenda kadhaa ikiwamo ya uchaguzi mkuu.

Bosi huyo wa Simba pia aliwashukuru viongozi kadhaa waliowahi kuongoza klabu hiyo akiwamo Ismail Aden Rage, Hasanoo na Mwina Kaduguda ambaye pia ni mjumbe wa bodi anayemaliza muda wake.

Kabla ya kuhutubia mkutano huo, Mangungu aliwaomba wanachama wa Simba kuwaombea wenzao waliotangulia mbele ya haki.

SOMA NA HII  BAADA YA KUAMBIWA YEYE NI TAJIRI WA INSTAGRAM..MO DEWJI AMJIBU MANARA KWA STAILI HII