Home Habari za michezo KUTOKA MKUTANO MKUU SIMBA: CEO MPYA AMRUDISHA KUNDINI BARBARA…AFUNGUKA KIKAO NAYE…

KUTOKA MKUTANO MKUU SIMBA: CEO MPYA AMRUDISHA KUNDINI BARBARA…AFUNGUKA KIKAO NAYE…

Mtendaji Mkuu wa Simba Iman Kajula kwenye Mkutano Mkuu leo

OFISA Mtendaji Mkuu mpya wa Simba, Imani Kajula amesema mtangulizi wake, Barbara Gonzalez bado hajaondoka kwenye klabu hiyo na wanaendelea kushirikiana.

Akizungumza mbele ya Wanachama waliojitokeza kwa wingi katika mkutano wa kawaida wa klabu unaokwenda sanjari na chaguzi mkuu hii leo kwenye ukumbi wa Mikutano wa Mwalimu Nyerere, Kajula amesema Barbara ataendelea kuwa mtu muhimu kwao.

“Jana niliwasiliana naye na Jumatano tumepanga kukutana ili kujadili mambo mbalimbali, lengo ni kuhakikisha tunapiga hatua zaidi.”

Kajula aliteuliwa Januari 26, mwaka huu alichukua nafasi ya Barbara Gonzalez aliyejiuzulu Disemba 10 mwaka jana.

Kajula ni mwanachama wa muda mrefu wa Simba na mbobezi katika masuala ya Kibenki na masoko akiwa na uzoefu wa kutosha aliouvuna akihudumu katika taasisi mbalimbali.

Pia ni mzoefu kwenye masuala ya uongozi wa mpira kwani alikuwepo kwenye Kamati ya Maandalizi ya Michuano ya Afrika kwa vijana chini ya umri wa miaka 17 (AFCON U17) iliyofanyika nchini mwaka 2019.

SOMA NA HII  KWA JERO TU..... SHABIKI WA SIMBA ASHINDA MAMILIONI JAKCPOT YA 10bet ....