Home Habari za michezo WAKATI CHAMA NA PHIRI WAKIPEWA SIFA…MGUNDA AIBUKA NA KUANIKA HILI KUHUSU KUIFUNGA...

WAKATI CHAMA NA PHIRI WAKIPEWA SIFA…MGUNDA AIBUKA NA KUANIKA HILI KUHUSU KUIFUNGA COASTAL JUZI….

Kaimu Kocha Mkuu wa Simba, Juma Mgunda amesema kuwa licha ya kuibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Coastal Union, lakini ilikuwa mechi ngumu ambayo iliamuriwa na uzoefu wa wachezaji wake.

Mchezo huo uliochezwa kwenye Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga, Simba ilipata mabao yake dakika ya 53 na 61 yaliyofungwa na Moses Phiri aliyefikisha mabao 10 kwenye orodha ya wafungaji sawa na Fiston Mayele.

Clatous Chama alihitimisha ushindi wa Simba dakika ya 89, huku likiwa bao lake la pili msimu huu ambapo hadi sasa amechangia upatikanaji wa mabao tisa akifunga mawili na kutoa pasi saba za mabao.

Akizungumza baada ya mchezo Kocha Juma Mgunda, alisema kuwa ulikuwa mchezo mgumu kwani alikutana na vijana aliowakuza kisoka lakini alikuja kama muajiliwa wa Simba na lengo lake ni kutimiza mipango ya waajili wake kwa kufikia malengo waliyojiwekea msimu huu.

“Mechi ilikuwa ngumu sababu vijana wengi nawajua uwezo wao na upambanaji wao ndio maana hata dakika 45 zilikuwa ngumu lakini tulichoenda kuzungumza kwenye chumba cha kubadirishia nguo ndio kimeamua mchezo.”

SOMA NA HII  ALPHONCE MABULA MBONGO ANAYESUMBUA ULAYA...WAZUNGU WAMFANANISHA NA TRENT WA LIVERPOOL..