Home Habari za michezo ZA NDAANIII…WACHEZAJI SIMBA WALIVYOHUSIKA NA KUJIUZULU KWA BARBARA…

ZA NDAANIII…WACHEZAJI SIMBA WALIVYOHUSIKA NA KUJIUZULU KWA BARBARA…

Kikosi cha Simba SC Msimu huu wa 2022/23

Siku cheche tangu CEO wa Simba SC, Barbara Gonzalez atangaze kuachia wadhifa huo ifikapo Januari 2023, Taarifa za chini chini kutoka ndani ya klabu ya Simba juu ya sakata la kujiuzulu kwa Afisa Mtendaji mkuu wa Simba SC, Barbara Gonzalez zinadai kuna Wachezaji walipiga kura ya siri kumkataa mwanamama huyo.

Inadaiwa Barbara alifanya mambo yafuatayo akiwa katika nafasi yake kama Mtendaji Mkuu;

Wachezaji wa Simba SC walipiga kura ya maoni na wengi walichagua CEO huyo aachie ngazi. Inadaiwa Barbara aliondoa baadhi ya posho ndani ya klabu hiyo.

Mwanamama huyo anadaiwa kuongeza matumizi na shughuli binafsi. Barbara alikuwa hataki wachezaji kumtembelea hata kwa shida binafsi.

Simba imepoteza wachezaji na makocha wazuri chini ya Afisa Mtendaji huyo kwa kwanza Mwanamke katika historia ya vilabu Tanzania.

SOMA NA HII  SIKU MOJA BAADA YA KUPEWA UKOCHA TAIFA STARS...MEXIME AAMUA KUFUNGUKA YA MOYONI..."HATUTAONGEZA MTU"...