Home Habari za michezo KOCHA MPYA SIMBA SC APANIA MAKUBWA AFRIKA…HUO MSHAHARA WAKE KUFRU TUPU…

KOCHA MPYA SIMBA SC APANIA MAKUBWA AFRIKA…HUO MSHAHARA WAKE KUFRU TUPU…

Kocha Mkuu Simba SC

Kocha Mkuu wa Simba SC Robertinho mesema siku zote anawaza vitu vikubwa na malengo yake ni makubwa ikiwemo kufika Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Robertinho ambaye amesaini mkataba wa miaka miwili wa kuifundisha Simba SC amesema watu wengi wamekuwa wakifikiria kuhusu hatua ya makundi lakini ukiweka mipango mizuri hata fainali inawezekana.

Kuhusu ubingwa wa Ligi Kuu, Robertinho amesema yeye ni mshindani na anaamini katika mipango dhabiti hivyo kila kitu kinawezekana.

“Nimewahi kuwa mchezaji kabla ya kuwa kocha, siku zote naamini katika mipango mizuri. Ukiwa na mipango mizuri unaweza kufika nusu fainali mpaka fainali hilo linawezekana pia nikiwa hapa Simba SC.

“Wakati niko Vipers tulipokuwa tunaenda kukutana na TP Mazembe wengi waliamini ulikuwa mwisho wetu lakini tulikuwa na mipango mizuri mpaka tukafanikiwa kuwatoa,” amesema Robertinho.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Simba SC, Murtaza Mangungu amesema kitu kilichotuvutia kwa Robertinho ni ubora na uzoefu wake kwa soka la Afrika Mashariki kwa hiyo tunaamini atatufikisha tunapopataka.

“Robertinho ni kocha mwenye wasifu mkubwa nasi tuna malengo makubwa ndiyo maana tumemchukua, ana uzoefu mkubwa wa soka la Afrika Mashariki hilo pia limetuvutia,” amesema Mangungu.

Taarifa za chanzo chetu cha kuaminika kinasema kuwa, Kocha huyo atakuwa akilipwa mshahara wa dola 10,000 kwa mwezi sawa na Milioni 23 za kitanzania.

Pamoja na mshahara huo atakuwa akipewa bonasi ya laki tano kwa kila mechi atakayoshinda, pamoja na marupurupu ya milioni 1 kila mwezi kwa ajili ya kumrahisishia maisha yake.

Pia amekabidhiwa nyumba ya kisasa pamoja na gari kwa ajili ya matumizi yake ya kila siku.

Aidha, atapewa bonasi ya milioni 10 endapo Simba SC watabeba ubingwa wa ligi kuu na makombe yote ya ndani, huku akipewa milioni 23 endapo Simba watafuzu kucheza robo fainal ya Ligi ya Mabingwa Afrika, endapo ataipeleka Fainal dau hilo litapanda.

Kwa upande mwingine mkataba wa kocha huyo utavunjwa endapo atashindwa kuiingiza timu hiyo hatua ya makundi ya klabu bingwa Afrika kwa msimu ujao.

SOMA NA HII  BENKI YA NBC WAKATA MZIZI WA FITINA KUHUSU UDHAMINI WAO LIGI KUU...WATOA TAMKO HILI LEO....