Habari za Simba
Habari za michezo

HIVI NDIVYO BACCA ANAVYOIVURUGA ILE YANGA ILIYOZOELEKA…..JOB HUENDA AKAISHIA BENCHI DAIMA…

admin April 6, 2023 8:19 am

Namuona Djuma Shabani akirudi katika nafasi yake kwa sababu ya uwezo wake mkubwa wa kushambulia.

Ni hapo ndipo ambapo Kocha Nabi atalazimika kuchukua uamuzi mgumu. Atamuweka nje Job au atamuweka katika nafasi ya Mwamnyeto?

Sioni kama Bacca atakaa nje kutokana na ubora ambao anauonyesha hewani na miguuni. Nabi atalazimika kufanya uamuzi mgumu. Lakini zaidi kuimarika kwa Bacca huku pia Mwamnyeto akiwa amerejea na Job angali akiwa imara kunasababisha sasa Yannick Bangala arudi katika nafasi yake anayoipenda kuitumikia. Nafasi ya kiungo.

Hili nalo litaleta vurugu katika eneo hili kwa sababu Yannick ataenda kuungana na Sure Boy, Khalid Aucho, Mudathir Yahaya, Gift Mauya na Aziz Ki kwa mbele yao.

Kichwa kitakuwa kinamuuma Nabi namna ya kupanga kikosi. Hata hivyo, kwa namna moja au nyingine hii ndio faida ya kuwa na wachezaji wengi bora katika kikosi kimoja.

Si ajabu ndio maana Yanga wanafanya vizuri katika michuano mbalimbali ambayo wanashiriki kwa sasa.

CAF YAIRUDISHA SIMBA MOROCCO…KUVAANA NA WAKALI HAWA ROBO NABI AWACHANA RIVERS UNITED…AWAPANIA HASWAA…AMEZUNGUMZA HAYA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply