Home Habari za michezo YANGA SC WAIFANYIA UMAFIA SIMBA KWA MUDATHIRI…WAMPA MKATABA WA FEI TOTO…

YANGA SC WAIFANYIA UMAFIA SIMBA KWA MUDATHIRI…WAMPA MKATABA WA FEI TOTO…

Habari za Yanga SC

BAADA ya Wananchi kusubiri sana, hatimaye vyuma vimeanza kutua. Na tunaposema vyuma, tunamaanisha vyuma kweli kweli.

Kiungo chuma, Mudathir Yahya ni mali ya Yanga SC baada ya Mzanzibar huyu kusaini mkataba wa kuwatumikia Wananchi.

Mkataba huo ulisainiwa mchana leo mbele ya Rais wa Klabu ya Yanga SC, Eng. Hersi Said na mtendaji mkuu Andre Mtine

Baada ya kusaini mkataba huo, Mudathir alipanda boti na kuelekea Zanzibar kwa ajili ya kujiunga na kikosi cha Yanga SC kwa ajili ya mashindano ya Kombe la Mapinduzi.

Kwa muda mrefu , Mudathir alikuwa akihusishwa na Simba SC , ambapo vyanzo vya karibu vinadai kuwa kiungo huyo alikuwa karibu kusaini dili na wekundu hao wa msimbazi kabla ya mambo kuja kuharibika dakika za miwshoni.

Mudathiri amesaini mkataba wa kuichezea Yanga SC kwa miaka miwili huku ikidaiwa kuwa atakuwa akilipwa Milioni 4 za kitanzania kama mshahara wake wa mwezi.

Kiungo huyo sasa ni wazi anaenda kuungana na swahiba wake kutoka Azam FC, Salum Abubakar ‘Sure Boy’ ambaye alijiunga jangwani msimu uliopita.

SOMA NA HII  AHMED ALLY: KAMA TUTAENDELEA HIVI UBINGWA SIMBA TUSAHAU...TIMU YETU BADO SANA ...