Home Habari za michezo KIUNGO YANGA SC ATIMKIA ZAKE LIBYA…ISHU NZIMA IKO HIVI….

KIUNGO YANGA SC ATIMKIA ZAKE LIBYA…ISHU NZIMA IKO HIVI….

Kikosi cha Yanga SC

Kiungo wa zamani wa Yanga SC, Haruna Niyonzima wiki hii atasafiri kwenda Libya kuanza kazi rasmi kwenye timu yake mpya ya Al Ta’awon inayoshiriki Ligi Kuu nchini humo aliyosaini mkataba wa mwaka mmoja.

Nyota huyo aliyesajiliwa na Yanga SC mwaka 2011 kabla ya kujiunga Simba mwaka 2017 kwa sasa anakipiga AS Kigali alipojiunga nayo baada ya kuagwa rasmi na Yanga mwaka juzi siku ya mechi ya Ligi Kuu kati ya Yanga SC na Ihefu iliyolazwa mabao 2-0, yote yakifungwa na Feisal Salum ‘Feitoto’.

Niyonzima wa nje aliyechukua mataji mwngi ya Ligi Kuu Tanzania. Juzi kiungo huyo aliyekua nahodha wa Timu ya Taifa ya Rwanda, aliagwa rasmi na AS Kigali akitakiwa kila la heri katika majukumu yake mapya ambaypo anaenda Libya.

Alipotafutwa Niyonzima kuzungumzia hilo alisema tumpe muda na kuanzia leo kila kitu kitakuwa sawa na watu watajua.

“Mpira ndio kazi yangu na siwezi kustaafu kuna sehemu naenda, naomba tuwe watulivu kidogo na siku si nyingi nitawajuza wapi naenda,” alisema Haruna anayesifika kwa kupiga pasi zenye macho.

SOMA NA HII  KISA MWANAYE KUSAINI YANGA...BABA'KE SURE BOY ASHINDWA KUJIZUIA..ADAI SIO SHABIKI WA YANGA...