Home Habari za michezo ACHANA NA SAIDOO…CHUMA HIKI KINGINE CHA MAANA KUTUA SIMBA SC…MBRAZILI KAMPITISHA..

ACHANA NA SAIDOO…CHUMA HIKI KINGINE CHA MAANA KUTUA SIMBA SC…MBRAZILI KAMPITISHA..

Habari za Simba

Mabosi wa Simba SC waliwasapraizi mashabiki wa klabu hiyo kwa kumsajili na kutambulisha kiungo mshambuliaji, Saido Ntibazonkiza ambaye mechi ya kwanza tu akiwa na timu hiyo alifunga hat trick na kuasisti moja, kisha siku chache wakajulishwa juu ya beki Henock Inonga kusaini mkataba mpya.

Kabla furaha ya mashabiki hao wa Simba C haijamalizikia, mabosi hao wakamtambulisha Mbrazili, Roberto Oliveira ‘Robertinho’ kuwa kocha mkuu mpya na fasta wakampandisha boti kwenda Zanzibar na juzi alishuhudia timu hiyo ikimaliza mechi ya kukamilisha ratiba ya Kundi C katika michuano ya Mapinduzi dhidi ya KVZ kwa kuifunga bao 1-0 awali aliishuhudia ikichapwa bao 1-0 na Mlandege.

Wakati mashabiki hao wakisikilizia na kutaka kuona Mbrazili huyo akianza kazi ya kukinoa kikosi hicho kinachoshika nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi Kuu, leo tena wanaletewa fundi mwingine mpya wa kuiimarisha timu hiyo inayojiandaa na mechi za makundi za Ligi ya Mabingwa.

Fundi huyo mpya ni kocha kutoka Tunisia ambaye anakuja kumsaidia Robertinho na kuimarisha benchi la ufundi lenye Juma Mgunda na Seleman Matola.

Chanzo cha taarifa kinasema kwamba kocha huyo amekuwa akifanya kazi na Robertinho katika klabu tofauti zikiwamo Stade Tunisien, Rayon Sports na Vipers, japo ujio wake umefanywa siri na mabosi wa Msimbazi.

“Kesho (leo) tunatarajia kumpokea mtaalamu mwingine kwa ajili yua kuimarisha benchi la ufundi la kocha Robertinho. Kocha aliyewahi kufanya kazi na Mbrazili katika timu tofauti lakini mwenye uraia wa Tunisia,” kilisema chanzo hicho na kuongeza;

“Ni kocha mwenye uwezo mkubwa, lakini makocha waliopo yaani Mgunda na Matola wataendelea kufanya kazi na Robertinho, kwani amewataka wote awe nao, japo kwa Matola inaweza kuwa ngumu kwa vile bado anaendelea na masomo yake ya kusaka Leseni A ya CAF na hivi karibuni iliripotiwa kuwa alibadilishiwa majukumu.”

Awali mabosi wa Simba SC walikuwa na hofu ya kumruhusu Robertinho kuja na wasaidizi aliofanya nao kazi katika klabu nyingine kwa hofu ya kupigwa na kitu kizito kama walivyofanyiwa na Zoran Maki ambaye alikaa klabuni hapo kwa siku chache na kutimka na wasaidizi wake aliowaleta, Kocha wa viungo Sbai Karim na wa makipa Mohammed Rachid kwenda Al Ittihad ya Misri.

Mwanaspoti limejaribu kuchimba kulipata jina la kocha huyo mpya Mtunisia aliyefanya kazi na Robertinho, lakini ilikwamba kwani chanzo kiligoma kabisa kulitaja kwa madai wanataka kufanya sapraizi kwa mashabiki wa klabu hiyo.

Hata hivyo, baadhi ya makosa waliowahi kufanya kazi na Robertinho akiwa Vipers ni pamoja na Mreno, Marcelo Carboso ambaye awali ilitajwa ndiye angekuja naye kabla ya kufahamika jana anakuja Mtunisia.

SOMA NA HII  MANJINAACHIWA NA TAKUKURU, NDANI YA CHAMPIONI JUMAMOSI