Home Habari za michezo BAADA YA MUDATHIR YAHAYA…JEMBE LINGINE LINALOTUA YANGA HILI HAPA….NABI ABARIKI….

BAADA YA MUDATHIR YAHAYA…JEMBE LINGINE LINALOTUA YANGA HILI HAPA….NABI ABARIKI….

Habari za Yanga SC

Kocha Mkuu wa Yanga ameanza mapumziko ya siku chache nchini kwake Ubelgiji baada ya kuugua kwa siku chache tangu alipomaliza mchezo wa mwisho wa ligi lakini kama unadhani jamaa amemaliza usajili unakosea.

Nabi amezungumza kwa njia ya simu akiwa kwake akisema baada ya uongozi wake kufanikisha usajili wa kiungo Mudathir Yahaya, sasa anahitaji straika mwingine wa mabao.

Kocha huyo aliyeshikilia rekodi nzito ya kupoteza mechi tatu pekee ndani ya misimu miwili alisema bado anadhani timu yake inauhitaji wa kupata mpachika mabao mwingine kando ya mfungaji wao kiongozi Fiston Mayele.

“Fiston (Mayele) anafanya vizuri sana lakini sio salama kuishi kwa kutegemea nguvu ya mtu mmoja lolote linaweza kutokea kwake ni lazima tuwe na chaguo lingine,”alisema Nabi.

“Kuna Clement (Mzize) lakini bado ni kijana ambaye tunatakiwa kumkuza vizuri na taratibu lakini hata kama tutamrudisha Yacouba(Sogne) haitakuwa haraka kurudi katika makali yake anahitaji mechi zaidi.

Nabi alisema tayari anafahamu mabosi wake wameshaanza kazi ya kusaka mshambuliaji huyo haraka katika kuboresha kikosi chao kabla ya kuanza kwa mechi za makundi za Kombe la Shirikisho Afrika.

Alisema katika kusaka mshambuliaji huyo ametaka mtu Bora ambaye anajua kufunga zaidi ya Mayele au kama Mkongomani huyo.

“Naamini tunaweza kumpata nawaamini viongozi wangu wana koneshkeni na watu wengi, tunahitaji mtu kama Mayele au zaidi yake ili tuwe na chaguo la kutosha katika eneo hilo.

Yanga imekuwa ikipata shida kushinda kwa urahisi anapokosekana Mayele ambapo mara nyingi wamekuwa wakibebwa na kiungo Feisal Salum ‘Fei Toto’ ambaye naye anataka kutimka katika timu hiyo.

Hata hivyo, mtihani kwa Yanga hata kama itampata mshambuliaji huyo watalazimika kuondoa majina ya mastaa wa kigeni waliopo sasa kufuatia idadi ya wachezaji wa kigeni kutimia.

SOMA NA HII  MUONEKANO WA UKURASA WA MBELE GAZETI LA CHAMPIONI JUMATANO