Home Habari za michezo YA FEI TOTO YANUKIA SIMBA…MKWANJA ANAOKUNJA PETER BANDA NI KUFRU TUPU…

YA FEI TOTO YANUKIA SIMBA…MKWANJA ANAOKUNJA PETER BANDA NI KUFRU TUPU…

Habari za Simba

Jarida la African Fact Zone limemuweka winga wa klabu ya Simba na timu ya taifa ya Malawi, Peter Banda kuwa analipwa mara tano ya mshahara wake wa kwanza ambao alikuwa akilipwa katika klabu ya Moldova ambayo ilikuwa ni FC Sheriff Tiraspol.

Jarida hilo limeuweka wazi mshahara wa winga huyo wa klabu ya Simba na kusema kuwa analipwa dola 4,000 ambazo ni sawa na Tsh 9,340,000/= yaani milioni Tisa laki tatu na arobaini elfu kwa mwezi.

Kwa mujibu wa tarifa yao waliyoichapisha Twitter kuwa analipwa mara tano kwa maana hiyo mshahara wa Banda mwanzoni ulikuwa ni dola 800 ambazo ni sawa na Tsh 1,868,000/= milioni moja na laki nane sitini na nane elfu.

Ada yake ya usajili kwenda simba ilikuwa dola 24,000/ sawa na Tsh milioni 56.

Pamoja na kulipwa malipo hayo makubwa, bado staa huyo wa Malawi, ameshindwa kuonyesha kiwango kikubwa kama ilivyotarajiwa tofauti na baadhi ya nyota wazawa wanaokipiga ndani ya timu hiyo ambao wanalipwa mshahara chini ya hapo.

Katika uchunguzi wetu, imeeonekana kuwa, Banda anawazidi mbali mastaa wazawa wanaoanza kwenye kikosi cha kwanza, kama Mzamiru Yassin ambaye inasemekana analipwa Milioni 4.

Wengine ni pamoja na Kibu Denis anayedaiwa kulipwa milioni 3, John Bocco anayedaiwa kulipwa Milioni 5, na wengine wengi ambapo kwa  wachezaji wa kitanzania anayeongoza kulipwa mshahara mkubwa ni Aish Manula anayelipwa Milioni 10 kulingana na mkataba mpya aliousaini mwaka jana.

Wengine, ni Mohamed Husein Mil 8, Shomari Kapombe Mil 7.5, wakati mastaa wengine wote wakitanzania hakuna anayevuka mshahara wa Milioni 4 kwa mwezi.

Hili linaweza kuzaa tafrani kama ilivyotokea upande wa pili wa Yanga, ambapo Feisal Salum ‘Fei toto’ alipovunja mkataba wake na klabu hiyo kwa kile kilichodaiwa kupata maslahi madogo kuliko mastaa wengine wa kigeni ambao hawana ‘impact’ kwenye timu.

SOMA NA HII  AUCHO NI MAJANGA JUU YA MAJANGA YANGA....ISHU NZIMA IKO HIVI...