Home Habari za michezo PAMOJA NA KUWA IHEFU….’JINAMIZI’ LA SIMBA LAZIDI KUMSUMBUA OKWA…AFUNGUKA A-Z…

PAMOJA NA KUWA IHEFU….’JINAMIZI’ LA SIMBA LAZIDI KUMSUMBUA OKWA…AFUNGUKA A-Z…

Habari za Simba

BAADA ya kupata nafasi ya kuitumikia Ihefu FC, kwa mkopo winga, Nelson Okwa amesema ni nafasi yake kuhakikisha anapata nafasi ya kucheza kikosi cha kwanza na kuisaidia timu hiyo kubaki Ligi Kuu Bara.

Okwa amejiunga na Ihefu kwa mkopo wa mwaka mmoja akitokea Simba ambayo hakuwa na namba kikosi cha kwanza tangu amejiunga na timu hiyo akiifungia bao moja tu kwenye mchezo wa kirafiki dhidi ya St George wakiibuka na ushindi wa mabao 2-0.

Okwa alisema ameyapokea maamuzi hayo kutoka kwa viongozi wa Simba na anaamini kwenye kikosi chao alikosa tu nafasi ya kucheza lakini bado ana nafasi ya kufanya vizuri Ihefu na kuisaidia kupata matokeo mazuri ambayo yatawafanya wabaki Ligi Kuu.

“Sio kitu kibaya ni kizuri kwangu kwa sababu nilikuwa nahitaji nafasi ya kupata timu ya kucheza kikosi cha kwanza naamini kwa upande wangu nina kazi ya kufanya ili kuwaaminisha wadau wa mpira kuwa nina uwezo wa kufanya vizuri na natamani kucheza mzunguko wote wa pili kwa mafanikio makubwa,” alisema na kuongeza;

“Kutolewa kwa mkpo haina maana kwamba sina uwezo wa kucheza siyo kweli nimekosa nafasi ya kucheza kikosi cha Simba huku nilipo sasa naamini nina kila sababu ya kujihakikishia namba kikosi cha kwanza ili nifanye kazi yangu kwa ubora.”

Okwa alisema anatamani kuwa mchezaji bora kwenye sajili zote zilizofanyika dirisha dogo kutokana na kukaa nusu msimu kwenye timu kubwa bila kuonyesha kutokana na kukosa nafasi hataki kurudia makosa.

“Nimetoka Simba timu kubwa ambayo inafanya vizuri pamoja na kuto kucheza haina maana kwamba usajili wangu haukuwa na maana ndani ya timu ni kukosa nafasi ya kucheza naamini ili kuonyesha kuwa hawakubahatisha ni kuwa bora.”

SOMA NA HII  KISA MECHI ZA 'NDONDO'....SHAFIIH DAUDA 'AMPA ZA USO' RAIS WA TFF...ADAI HATA YEYE ALICHEZA KABLA HAJAWA RAIS...