Home Habari za michezo BANGALA NA DODOMA JIJI SASA MAMBO NI MUSWANO….KUANZA KUVAA JEZI YAO RASMI…

BANGALA NA DODOMA JIJI SASA MAMBO NI MUSWANO….KUANZA KUVAA JEZI YAO RASMI…

Habari za Usajili TZ

Uongozi wa Dodoma Jiji umekamilisha vibali vyote vya nyota wake, Randy Bangala aliyekuwa nje ya uwanja kwa muda mrefu tangu ilipomsajili Julai 7, mwaka jana akitokea timu ya AS Maniema Union.

Akizungumza nasi jijini Dar es Salaam katibu mkuu wa kikosi hicho, Fortunatus Johnson alisema kila kitu kimekamilisha kwa nyota huyo raia wa Congo na kilichobaki ni benchi la ufundi kumtumia.

“Shida ilikuwa ni kupata kibali chake cha uhamisho wa kimataifa (ITC) katika klabu aliyotokea ya Maniema Union hivyo tunashukuru kwani kila kitu kipo sawa,” alisema Fortunatus na kuongeza;

“Mashabiki wetu walikuwa na hamu sana ya kumuona uwanjani na sisi kama viongozi shauku kubwa ni kuona anaanza kukitumikia kikosi chetu kwa sababu ataongeza ushindani wa nafasi kwa waliopo.”

Kwa upande wa Bangala ambaye ni mdogo wake na mchezaji wa Yanga, Yannick Bangala alisema furaha yake ni kuona anacheza na kukata kiu ya mashabiki zake waliokuwa wanatamani kumuona uwanjani.

“Mimi nafanya mazoezi na wachezaji wenzangu na najiona niko fiti kucheza hivyo jukumu nawaachia benchi la ufundi,” alisema.

Mbali na kuichezea Maniema ila Bangala amewahi kuchezea timu mbalimbali za TP Les Croyant, FC Renaissance, Jeunesse Sporting Tsangu ambazo zote kwa pamoja zinapatikana nchini kwao Congo.

SOMA NA HII  USAJILI WA AZIZ KI NA NAMNA YANGA WALIVYOTUMIA MBINU ZA KIMAFIA KUMFICHA ASITEKWE NA SIMBA...

1 COMMENT