Uncategorized

HAWA NDIO UD SONGO WAPINZANI WA SIMBA KIMATAIFA, UKIWAPIGA MAPEMA WANAPOTEANA MAZIMA

admin August 10, 2019 7:34 am


 UD Songo ya Msumbiji msimu uliopita walishiriki michuano ya Ligi ya Mabingwa na kutupwa nje na Nkana FC ya Zambia ambayo nayo ilipigwa chini na Simba.

Sasa leo wapo kazini kwenye mchezo wa awali dhidi ya Simba utakaochezwa nchini Msumbiji. 

Kwenye mechi 14 za ligi ambazo wamecheza wameshinda jumla ya mechi 8 wamelazimisha sare mechi mbili na kupoteza mechi 4.

UD Songo ni timu inayofanya counter attack nyingi na wana kasi ya hali ya juu. Hivyo Simba leo lazima kuwa makini kuwadhibiti kwa kuwawahi mapema.

Hata hivyo msimu uliopita haikuwa hatari katika umaliziaji kwa kuwa ilikosa washambulizi bora na wazoefu.

Msimu huu kikosi hicho kimefanya marekebisho kadhaa wakiwa na nia ya kufika mbali kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika karata yao ya kwanza ni leo mbele ya Simba wakiwa nyumbani kwao.

NYOTA SITA WA YANGA HAWA HAPA HATIHATI KUIKOSA TOWNSHIP ROLLERS LEO YANGA, SIMBA, KMC AZAM FC WAPINZANI WENU NI VISIKI ILA WANAFUNGIKA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6131

Leave a Reply