Home Habari za michezo MANARA ALIAMSHA KWA MASHABIKI WA YANGA….’AWAPA ZA USO LIVE’…

MANARA ALIAMSHA KWA MASHABIKI WA YANGA….’AWAPA ZA USO LIVE’…

Habari za Yanga

Aliyekuwa msemaji wa Klabu ya Yanga, Haji Manara, ameeleza kuwa haridhishwi na idadi ya mashabiki wanaojitokeza kushuhudia mechi za timu hiyo.

Manara leo ameandika; “Washabiki wa Yanga  tunapaswa kujibidiisha kwenda Uwanjani ili kuhanikiza ushindi wa leo.

“Hatupaswi kuishia mitandaoni tu na kutambia ubora wetu tulio nao, kiukweli binafsi siridhishwi na namba ya mashabiki wakati huu timu yetu inafanya vizuri na tunaongoza ligi.

“Sasa kila mmojqa kwa nafasi yake amhimize mwenzie kuja uwanjani kwa mkapa, imagine mikoani wanawashinda watu wa Dar kupendezesha uwanja,” amesema Manara.

Yanga itashuka kwenye dimba la Benjamin Mkapa siku ya Jumapili, majira ya saa 1:00 jioni kupambana na Rhino Rangers kwenye mchezo wa Hatua ya 32 b Kombe la Shirikisho la Azam.

SOMA NA HII  GAMONDI AFANYA MAAMUZI MAGUMU KWENYE KIKOSI CHA YANGA, MAYELE ATAJWA