Home Habari za Simba HUYU BALEKA SIMBA WASIPOMUANGALIA HUYU…UNAAMBIWA KAANZA KUTAKA MAMBO MAKUBWA

HUYU BALEKA SIMBA WASIPOMUANGALIA HUYU…UNAAMBIWA KAANZA KUTAKA MAMBO MAKUBWA

Habari za Simba

Straika mpya wa Simba, Jean Baleke amesema anaamini anaweza kuonyesha kiwango bora zaidi ya alivyocheza mchezo wa kwanza wa kimashindano ndani ya timu hiyo na kuwataka mashabiki wampe muda.

Baleke alisema hakupata muda wa kutosha kufanya mazoezi na wachezaji wenzake wote, bado hajazoea mazingira ndani ya Simba na hata nje ya timu pamoja na mambo mengine lakini atarudi kwa moto zaidi.

Alisema ameona watu haswa mashabiki wa Simba wamefurahi baada ya kufunga bao kwenye mechi ya kwanza walipowachapa Dodoma Jiji bao 1-0, ila anaamini kwenye uwezo wake anaweza kufanya zaidi ya vile alivyofanya kwa kuwa anajua ana uwezo mkubwa zaidi.

“Nashukuru Mungu amenipa uwezo wa kufunga kama nikipata muda wa kutosha kufanya mazoezi na kuzoea mazingira ya timu nitafanya vizuri zaidi ya ilivyokuwa mchezo wa kwanza mashabiki wa Simba wasiwe na hofu nami wanachotakiwa kufanya ni kuhakikisha wananipa ushirikiano tu.

“Nikiitazama Simba naona ina wachezaji wengi bora, hili ndiyo jambo zuri, kwa muunganiko huu tutafanya vizuri sana kwenye michuano yote ile ya Afrika na hata ligi za ndani,” alisema Baleke na kuongeza;

“Jambo zuri kuwa na mwanzo mzuri kwangu mechi ya kwanza nimefunga bao muhimu kwa timu na kwenda kutupa pointi tatu ambazo tulikuwa tunazihitaji kuliko jambo lingine lolote.

“Naamini kuna kazi nzuri nimekuja kufanya hapa Simba na nitaongeza ubora wa timu haswa kwenye eneo la kufunga na hilo linawezekana kabisa.”

Baleke ambaye amejiunga na Simba kwenye dirisha hili amekuwa mmoja kati ya wachezaji ambao wamesajiliwa na kufunga kwenye mchezo wa kwanza, huku akisema muhimu kwake ni kuona timu inashinda.

“Jambo la muhimu ni timu kwanza, timu ikipata ushindi ndiyo jambo zuri kwangu na wengine kikosini, haya mengine ni mambo ya ziada tu lakini kwanza tupate pointi tatu mimi kufunga najua ni kazi yangu na nitaifanya ipasavyo,”

SOMA NA HII  KAMA HUU NDIO 'UBABU' WA ONYANGO, BASI SIMBA SC IMELAMBA DUME..!!