Home Habari za michezo HARUNA MOSHI ‘BOBAN’ vs CHAMA….NANI AANZE KIKOSI CHA SIMBA ….?

HARUNA MOSHI ‘BOBAN’ vs CHAMA….NANI AANZE KIKOSI CHA SIMBA ….?

Haruna Moshi Boban na Chama wote wachezji wa Simba

Simba wanae Clatous Chama kwenye eneo la kiungo mshambuliaji, Chama ni fundi wa mpira kweli anafanya kila kitu kwenye lile eneo anatimiza majukumu vyema akiwa kama kiungo mshambuliaji.

Tokea siku ya kwanza akiwa amevalia jezi ya Simba alianza kuimbwa kwa ufundi wake aliyoyafanya ni makubwa aliondoka lakini amerudi, Kwenye kiungo mshambuliaji yeye ni mwalimu mzuri, Achana na Mwamba wa Lusaka.

Zamani Simba waliwahi kuwa na kiungo mshambuliaji mwanadamu yule alikuwa fundi, Hakuwa anatokea Zambia,Ghana,Nigeria au Mali alikuwa ni fundi mmoja kutoka hapa hapa Tanzania tu.

Alifahamika kama Haruna Moshi miguu yake ilikuwa na ufundi ambao sitaweza kuuelezea ni kamaliza kwenye eneo la kiungo alipageuza kama nyumbani kwake utake nini Haruna Moshi asifanye.

Bukta yake ikiwa mlegezo lakini uwezo wake wa kuunganisha timu ulikuwa mkubwa sana pasi zake za kubembeleza kwa washambuliaji ile ball control,kufunga mabao vyote hivyo vikafanya apewe jina la Boban unamfahamu Boban?

Ukifika pale Italy, Waitaliano wenyewe walikuwa wanamuita Croatian Maestro ni Zvonimiri Boban fundi mmoja wa Croatia kwenye dimba la kati alichafua sana ni yeye aliyeiongoza Croatia kumaliza nafasi ya 3 pale Ufaransa wakati wa kombe la Dunia miaka ya 1998.

Haruna Moshi Boban aliingia kwenye ile Simba tamu ya Ulimboka Mwakingwe VCD,Joseph Kaniki Golota,Juma Kaseja ni 2004 hiyo. Haruna alijua kunyanyua watu majukwaani kwa ufundi wake mkubwa.

Mpira ulitumwa kila ulivyofika kwenye miguu ya Haruna,Akili yake ilijua nini cha kufanya kabla ya kupokea mpira kupoteza mpira haikuwa rahisi Haruna alikuwa kiungo kweli nyuma ya muda Simba walikuwa na mtu fundi sana.

Gefle If ya Sweden hawakusita kumsajili Haruna kutokana na ufundi miguuni mwake, Inawezekana angefanya makubwa kabla ya kina Samatta lakini haikuwa hivyo akarejea nchini.

Kwenye Simba ile yenye mapafu ya Patrick Mutesa Mafisango,juu kuna Afande Kazimoto. Haruna alikuwa kioo cha Simba wakina Okwi,Uhuru na Sunzu kazi zao ni kuuweka mpira wavuni tu. muda umetukimbia tuliwahi kuwa na Boban.

Dondosha maoni yako hapo chini, kati ya Haruna Moshi na Clatous Chama nani ni zaidi ya mwenzake kwa mtazamo wako, je wangekuwa wote wnaacheza zama moja na wewe ndiye kocha nani angenza kabla ya mwenzake?

SOMA NA HII  GOLI LA KIBRAZILI LAITAKATISHA SINGIDA BIG STARS MBELE YA TZ PRISONS...AMISI TAMBWE 'MIBICHWA' ATIKISA...