Home Habari za michezo KISA YANGA…BEKI LA CHAN LAKIMBIA MASHINDANO…AFUNGUKA UNDUGU WAKE NA SAIDO WA SIMBA…

KISA YANGA…BEKI LA CHAN LAKIMBIA MASHINDANO…AFUNGUKA UNDUGU WAKE NA SAIDO WA SIMBA…

Habari za Yanga

Beki mpya wa Yanga Mamadou Doumbia, amechukua maamuzi magumu yaliyoshtua akiitema kambi ya timu ya taifa lake kisha akawaaambia anakwenda kujiunga haraka na kambi ya klabu yake, kisha akachukua mabegi yake akatoka nje ya hoteli na kutimka.

Doumbia ni kati ya mastaa wa kigeni waliosajiliwa na Yanga katika dirisha dogo lililofungwa Jumapili usiku Januari 15, akija kuongeza nguvu katika ukuta wa vinara hao wa Ligi Kuu Bara.

Juzi mashabiki wa Yanga wakati timu yao inacheza na Ihefu walikuwa na maswali mengi jukwaani wakihoji staa huyo atatua nchini lini, lakini sasa jibu limepatikana.

Akizungumza  kwa njia ya simu, Doumbia alisema ameamua kuja haraka kujiunga na timu yake mpya akiwa na imani na mastaa wanaowaacha katika timu ya taifa lake.

Mali ilicheza mchezo wake wa kwanza juzi Januari 16 dhidi ya Mauritania na kutoka sare ya mabao 3-3, huku Doumbia akikosekana katika mchezo huo.

“Jambo zuri ni klabu zote zimeelewana na shirikisho la Mali pia, nimeona niwahi haraka kujiunga na timu yangu mpya, nasubiria tiketi ya ndege ili nije Tanzania (juzi) alisema Doumbia.

Beki huyo mrefu aliongeza kuwa amefurahi kukiamilika kwa dili hilo ambapo anajipanga kuja kuwa na maisha mapya kusaka mafanikio sawa na kipa na raia mwenzake wa Mali Djigui Diarra.

“Nimefurahi kujiunga na Yanga hii ni klabu kubwa lakini nina ndugu zangu hapo Diarra na Kanoute (Sadio wa Simba), nafurahia kuona mafanikio yao tangu wamekuja hapo nahitaji kupita njia kama hiyo.”

SOMA NA HII  YANGA: BADO TUNAO UWEZO WA KUTWAA UBINGWA WA LIGI KUU BARA

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here