Home Habari za michezo MCHEZAJI MWINGINE TENA ATUMIA NJIA YA FEI TOTO KUTOKA YANGA…AANDIKA BARUA…

MCHEZAJI MWINGINE TENA ATUMIA NJIA YA FEI TOTO KUTOKA YANGA…AANDIKA BARUA…

Habari za Yanga

Wakati sakata la kiungo Feisal Salum ‘Fei Toto’ jana likitolewa maamuzi na Kamati ya Sheria na Hadhi ya Wachezaji, mshambuliaji nyota wa Mtibwa Sugar, Adam Adam ameandika barua ya kuvunja mkataba wake wa miezi sita uliobaki klabuni hapo.

Fei aliburuzwa na Yanga katika kamati hiyo ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) baada ya kuvunja mkataba kwa kulipa Sh112 milioni ambazo hata hivyo zimerudishwa na jana maamuzi yalitoka na kuamuliwa bado ni mchezaji halali wa Yanga.

Lakini kwa Adam amewaomba waajiri wake kuvunja mkataba ili akatafute changamoto sehemu mpya na taarifa kutoka kwa mtu wa karibu wa mchezaji huyo zilieleza kwamba ni kweli amefikia uamuzi huo ingawa bado viongozi wake hawajajibu chochote kuhusu hilo.

“Ni kweli anataka kutafuta changamoto kwenye timu mpya ingawa bado uamuzi wa mwisho juu ya hilo haujafanyika,” kilisema chanzo hicho ambacho hata hivyo hakikutaka kuwekwa wazi.

Kwa upande wa Adam, alipotafutwa na Mwanaspoti alisema hawezi kuzungumzia jambo hilo kwa sasa.

“Kama kutakuwa na jambo lolote jipya ambalo linanihusu basi mashabiki wangu watajua tu,” alisema.

Akizungumzia hilo, kocha msaidizi wa timu hiyo, Awadh Juma ‘Maniche’ alisema anaamini kila kitu kuhusu mchezaji huyo kitakamilika kwani wao kama benchi la ufundi bado wanamuhitaji.

Nyota huyo alijiunga na kikosi hicho akitokea Polisi Tanzania huku ikielezwa sababu kubwa ya kutaka kuvunja mkataba wake ni kwa ajili ya kujiunga na JKT Tanzania ambayo imemuwekea fedha nyingi.

SOMA NA HII  BAADA YA KUONEKANA KAMA WAMESHINDWA BEI YA AZIZ KI....AHMED ALLY AIBUKA NA TAMKO HILI...ADAI NI UHUNI KWA SIMBA...

3 COMMENTS

  1. I loved as mych as youu wiill receive caarried outt
    right here. Thhe sktch is attractive, youhr
    authored subject matter stylish. nonetheless, youu command gget gott
    ann imkpatience over that you wishh bee delivering tthe
    following. unwelll unuestionably colme further formewrly again since exactly the same nearly very often inside case youu shield this increase.

  2. With havin so muhh content ddo youu evcer ruun ibto any issues of plagorism or copyright infringement?

    My sjte hhas a lot oof unique content I’ve either creatfed myself or outsiurced
    but it seems a lot of iit iss popping it up alll ovwr the iternet witthout my agreement.
    Do yoou know anny techniques to hhelp stopp content freom being ripped off?
    I’d truly appreciate it.

    My webpage; Mi prima mesorprense

  3. Nice answerr back in return of this matter wth genuine arguments and describing
    everything oon the topic of that.

    My blog: red