Home Habari za michezo MGUNDA ASHINDWA KUJIZUIA YALIYOTOKEA SIMBA…AWATAJA WACHEZAJI WALIOHUSIKA….

MGUNDA ASHINDWA KUJIZUIA YALIYOTOKEA SIMBA…AWATAJA WACHEZAJI WALIOHUSIKA….

Kocha Msaidizi Simba SC

Kocha msaidizi wa Simba, Juma Mgunda amesema pamoja na kushindwa kutetea taji la Mapinduzi, anajivunia kutoa nafasi kwa nyota wake wote wanaokosa nafasi kikosi cha kwanza.

Simba imeondolewa kwenye mashindano hayo baada ya kushinda mchezo mmoja na kufungwa mmoja, ikikusanya pointi tatu kwenye Kundi C alilokuwa na KVZ na Mlandege iliyotinga nusu fainali.

Akizungumza mara baada ya mchezo dhidi ya KVZ juzi, Mgunda alisema hawakuwa na msimu mzuri kwenye mashindano hayo, lakini anafurahi ametoa nafasi kwa wachezaji wake ambao walikuwa hawana nafasi.

“Mpira ni mchezo wa wazi, naamini kila mmoja ameona kilichofanywa na wachezaji hao ambao wamekuwa wakikosa nafasi ya kucheza mara kwa mara kikosi cha kwanza, kwa upande wangu kuna vitu nimeona, nitavifanyia kazo.

“Siwezi kusema ni vitu gani nimeona kwa sababu hata wakati natoa nafasi kwa wachezaji hao sikusema sababu ya kwanini nimewapa nafasi, hivyo mazuri niliyoyaona nitayaboresha na mabaya pia nitayafanyia kazi,” alisema kocha huyo.

Mgunda alisema anashukuru alichokifanya hajakishuhudia mwenyewe akimtaja kocha Robertinho Oliveira kuwa ni miongoni mwa mashuhuda wa michezo yote miwili akiwa jukwaani ameona ubora na upungufu wa kila mchezaji.

Kocha huyo wa zamani wa Coastal Union, aliongeza pia kuwa kuna pengo kubwa kati ya timu inayoanza kikosi cha kwanza na cha pili, ndiyo maana wachezaji wamekuwa wakijirudia wale wale kwenye mechi za Ligi Tanzania Bara.

Katika hatua nyingine, Mgunda alikataa kuzungumzia juu ya ujio wa kocha mwingine msaidizi wa Oliveira, akisisitiza kuwa hata yeye hafahamu jambo hilo, zaidi ya kukubali kuwa yeye ni kocha msaidizi.

“Nimeajiriwa hapa kama kocha msaidizi, nafikiri hilo linafahamika, kama unaniambia kocha mpya kaja na msaidizi wake mimi ndiyo nakusikia wewe na mimi nitakuwa sifahamu majukumu yangu mapya sasa,” alisema Mgunda.

SOMA NA HII  HII HAPA SLOT YENYE UHAKIKA WA KUTOA MSHINDI WA MAMILIONI KILA SIKU...