Home Habari za michezo A-Z JINSI INJIA HERSI ALIVYOWATIMULIA VUMBI SIMBA KWENYE ISHU YA MUDATHIR….

A-Z JINSI INJIA HERSI ALIVYOWATIMULIA VUMBI SIMBA KWENYE ISHU YA MUDATHIR….

Habari za Yanga SC

Usajili wa kiungo fundi kutoka Zanzibar, Mudathir Yahya kutua Yanga  ni kama filamu flani ya kimafia kutokana na namna mabosi wa Jangwani walivyombeba kiungo huyo aliyekuwa akielekea kutua Msimbazi kukipiga Simba.

Kiungo huyo aliyewahi kuzitumikia Azam FC na Singida United kabla ya kurejea visiwani kuichezea KMKM, kwa sasa tayari yupo katika kambi ya Yanga na usiku wa jana alitarajiwa kuwa sehemu ya kikosi cha timu hiyo katika mechi dhidi ya waajiri wake wa zamani, maafande wa KMKM.

Mapema taarifa zilikuwa zinasema, kiungo huyo alikuwa mbioni kujiunga na Simba, lakini ghafla Yanga ilipindua meza kwenye usajili huku kukiwa na filamu moja kubwa ilipigwa kati ya rais wa klabu hiyo na kocha wa timu hiyo.

Iko hivi. Usajili wa Mudathir kama ulikuwa hufahamu umetumia siku mbili pekee kukamilika na haraka akawahishwa kambini kuanza kazi.

Ishu nzima ilianzia kwa kocha wa Yanga, Nasreddine Nabi ambaye alitaka kuongezwa kiungo wa kati anayejua kukaba bila kuchoka na kuwasilisha mahitaji hayo kwa mabosi wake ambao kumbe walishajua ‘mido’ huyo anatakiwa na watani wao Simba.

Hesabu zao za haraka wakaona kwamba kama Mudathir atatua Simba atakwenda kutengeneza kitu kizito katika safu yao kiungo na haraka wakakubaliana kumaliza dili hilo kimafia.

Hesabu za Nabi na Hersi ni kwamba kama Mudathir ataungana na Mzamiru Yassin au Sadio Kanoute basi watatengeneza kiungo imara cha ukabaji ambacho kitawasumbua.

Ishu hiyo akaachiwa yuleyule Injinia Hersi ambaye usiku kucha alianza kuwasiliana na meneja wa mchezaji huyo ambaye anaishi Marekani na mazungumzo kukamilika saa 10:00 alfajiri, ambapo haraka juzi Mudathir akatumiwa tiketi ya boti atue Dar es Salaam.

Hata hivyo, Hersi alishtukia kitu na kusaka mtu ambaye atafika nyumbani kwa kiungo huyo ambapo alipoamka tu akakuta kuna gari ndogo inamsubiri kumpeleka bandarini.

Alipotua Dar kazi ilikuwa moja tu kusaini haraka zoezi ambalo kufika saa 5:30 asubuhi lilishakwisha.

Msikiee Nabi

Nabi alisema: “Nampongeza sana rais (Hersi) kwa kufanya dili hili haraka.”

SOMA NA HII  NYOTA SIMBA AKUBALI KURUDI ALIPOTOKA...AKATAA DILI LA KWENDA KUCHEZA ZAMBIA...ADAI ATAWASHANGAZA WATU...