Home Habari za michezo USAJILI WA KWANZA WA MBRAZILI NDANI YA SIMBA HUU HAPA….ALIKUWA ANAKIPIGA ZNZ….

USAJILI WA KWANZA WA MBRAZILI NDANI YA SIMBA HUU HAPA….ALIKUWA ANAKIPIGA ZNZ….

Habari za Simba

Kikosi cha Simba tayari imetua Dubai, huku kocha mkuu mpya wa Simba, Roberto Oliveira ‘Robertinho’ ameondoka na jina la straika mmoja chipukizi anayekipiga vinara wa Ligi Kuu ya Zanzibar (ZPL), KVZ akitaka atua Msimbazi haraka afanye naye kazi.

Dogo huyo aliyemvutia kocha huyo raia wa Brazili huyo ni Michael Joseph aliyefunga bao pekee la Simba kwenye michuano ya Kombe la Mapinduzi 2023, anayekipiga kwa mkopo KVZ kutoka timu ya vijana wa Simba B.

Iko hivi. Kinda huyo aliwaomba maafande hao wanaoongoza msimamo wa ZPL aitumikie Simba kwenye michuano hiyo ya Mapinduzi na kucheza vyema mechi mbili za timu hiyo ikiwamo ya kwanza aliyoingizwa kipindi cha pili na Simba kupasuka bao 1-0 kwa Mlandege na ya juzi kuanza kikosi cha kwanza na kufunga bao la kichwa akimalizia krosi ya Augustine Okrah.

Kutoka na soka tamu alililolipiga kwenye mechi hizo mbili za Kundi C, limemvutia kocha Robertinho ambaye ameagiza fasta arudishwe kikosini kwenye dirisha dogo linalofungwa wiki ijayo, ili afanye kazi na mchezaji huyo.

Chanzo cha kuaminika kutoka Simba, kimeliambia Mwanaspoti kuwa Joseph atarudishwa haraka kwenye kikosi chao kutokana na Mbrazili kuhitaji huduma yake baada ya kumshuhudia akicheza michezo miwili mfululizo kwa kiwango bora, licha ya timu kutemeshwa taji ililokuwa ikilishikilia.

“Ni kijana wetu, yupo KVZ kwa mkopo. Tumeamua kumchezesha Simba kwa mujibu wa mkataba na hii ipo kwa wachezaji wote wakitolewa kwa mkopo, hawawezi kucheza dhidi yetu na kwa kuwa Mapinduzi inaruhusu kumtumia mchezaji yeyote ukiwahi kuwasilisha jina, ndio maana tulimchukua na kumpa nafasi ya kucheza,” kilisema chanzo hicho na kuongeza;

“Ni kama bahati kwake, kwani kocha kamuona na kupendezwa naye, hivyo kwa kutumia dirisha la usajili tutafanya mazungumzo na KVZ ili kumrudisha kikosini haraka kama ilivyotakiwa na kocha wetu mpya.”

Akizungumza na Mwanaspoti baada ya mchezo huo wa kukamilisha ratiba kwani Simba ilikuwa tayarin imeshaaga michuano mapema, Joseph alikiri kuifunga timu anayoichezea ilimuuma, ndio maana aliomba radhi mashabiki kwa kupunga mkono huu badala ya kushangilia.

“Mimi ni mchezaji wa KVZ, lakini nipo kwa mkopo sijajua makubaliano yalikuwaje wanatakiwa kuzungumza ni viongozi waeleze kwanini nimeichezea Simba na sio timu yangu ya mkopo, ila ninachoweza kusema nashukuru nimetekeleza kile nilitakiwa kukifanya.”

SOMA NA HII  KITAMBI FULL UBABE GEITA GOLD