Home Habari za michezo YANGA ACHENI KUMKOMOA FEI TOTO…VAENI VAZI LA UZAZI…MWACHENI AONDOKE

YANGA ACHENI KUMKOMOA FEI TOTO…VAENI VAZI LA UZAZI…MWACHENI AONDOKE

FEISAL SALUM

Yanga ni kubwa kuliko Fei, Yanga inafanya vizuri bila Fei., Yanga ipo robo fainali Kombe la Shirikisho Afrika bila Fei, Yanga ilikuwepo kabla ya Fei, Yanga itakuwepo baada ya Fei, Yanga ilishapata hasara
kubwa kuliko hii ya Fei….

Naamini itakua ni busara sana TFF kutenganisha ndoa ya Fei na Yanga!
Sawa, Kwenye mikataba hakuna huruma lakini wakati mwingine ukiona hupotezi kikubwa ni bora ukasamehe kidogo ili kulinda taswira yako kwa siku za mbele.

Kinyume na hapo itatafsiriwa kama kukomoana kitu ambacho sio kizuri kwa maslahi ya mchezaji na Taifa kwa ujumla.

Mchezaji hataki kuendelea kusalia Yanga, Yanga inachotaka kwa mchezaji husika ni ngumu kutokea!

Hakuna timu itakayotaka kumsajili Fei ikiwa ataendelea kusomeka kama mchezaji wa Yanga, kwa kuwa kufanya hivyo hiyo timu itaonekana ndio iliyomrubuni Feisal. Yanga wachukue issue ya Bernard Morrison kama Case Study kwenye hili sakata…

Kama Yanga wangeshinda kesi dhidi ya Morrison halafu wakachagua kumkomoa leo asingecheza dhidi ya Kagera Sugar na kufunga bao zuri!!

Hivi kuna dhihaka, kejeli na dharau wamewahi kukutana nayo Yanga kama kwenye ile kesi ya Morrison? Kuna matusi Yanga wamewahi kutukanwa kama kipindi Haji Manara yupo Simba?

Leo hawa wote wako Yanga na maisha yanaendelea… kwenye Mpira ukiweka kinyongo cha maisha utaumia buree. Au kwakuwa Feisal ni Mtanzania…?

Mchezaji kakosea ndio, lakini lazima busara itumike kuokoa kipaji chake! Busara ile iliyotumika kumpa Manara cheo wakati aliwahi kuwaambia kwamba wenye akili ni Baba yake na Mzee Kikwete hiyo hiyo itumike kumuachia Feisal Salum.

Busara ile iliyotumika kumrejesha Bernard Morrison aliewatia hasara na kuwavulia mpaka bukta akabaki na chupi pale Kigoma hiyo hiyo itumike kumuachia Feisal.

Mbona wenzenu Mzungu aliwakimbia na hatukuona kesi yoyote…? Maumivu mtakayoyapitia kumuacha Fei ndio hayo hayo Kambole, Yacouba na Bigirimana waliyapitia..

Shida iko wapi…?

Aziz Ki kaziba pengo vizuri na anapiga miwa na kuondoka na mpira hivyo hivyo kiungo chuma Mudathir Yahaya anakichafua pale katikati na uzuri zaidi Yanga wana Mwalimu mzuri…hofu yenu nini?

Muacheni Fei akacheze anapotaka!
Ameandika Sospeter llagila

SOMA NA HII  BAADA YA KUFUNGWA JANA...TUMAINI LA SIMBA QUEENS LIMEBAKIA HAPA SASA...WAKIFELI NI NCHI IMEFELI...