Home Habari za michezo HATIMAYE NABI AITUMIA MASHINE YAKE MPYA NI HATARI…TAKWIMU KAMILI HIZI HAPA

HATIMAYE NABI AITUMIA MASHINE YAKE MPYA NI HATARI…TAKWIMU KAMILI HIZI HAPA

HATIMAYE NABI AITUMIA MASHINE YAKE MPYA NI HATARI...TAKWIMU KAMILI HIZI HAPA

Kocha Mkuu wa Yanga Nasreddine Nabi juzi Aprili 11, 2023 alimtumia kwa mara ya kwanza beki Mamadou Doumbia katika mchezo wa ligi kuu ya NBC.

Doumbia aliingia dakika ya 67 kwenye mchezo dhidi ya Kagera Sugar ambao Yanga iliibuka na ushindi wa mabao 5-0 katika uwanja wa Azam Complex.

Doumbia alitumia takribani dakika 25 alizotumika katika mchezo huo akionyesha umahiri wake katika kupiga pasi, kunusa na kuokoa hatari pamoja na kucheza mipira ya juu.

Mara kadhaa Nabi aliweka bayana kuwa Doumbia hatumiki sio kwa sababu ni mchezaji mbaya, bali anampa muda ili aweze kuzoea mbinu ya aina ya uchezaji wa wenzake.

Wakati Doumbia anasajiliwa na Yanga, tayari aliwakuta wenzake wanafanya vizuri katika nafasi anayocheza hivyo ilikuwa ni lazima kwa Nabi kuwa na uvumilivu ili kuhakikisha hamuweki kwenye presha kubwa
Taratibu Doumbia ameanza kuonekana na bila shaka wale waliokuwa na mashaka nae watatulia.

Takwimu zake;
Dk. 23
25. Touches
10(10) passes
100% pass accuracy
01. Clearances
00. Blocks
01. Aerial Duels | high boll’s Won
Umekionaje kiwango cha Mamadou Doumbia Kwenye mchezo huo?

SOMA NA HII  KISA UWEPO WA SAKHO NA BANDA...WAPINZANI WA SIMBA CAF WAANZA KUPAGWA....WAAMUA KUJA NA MBINU ZA KIJASUSI...