Mshery golikipa wa Yanga
Habari za michezo

MSHERY ‘KUPIGWA KISU’ TUNISIA…YANGA WAAMUA LIWALO NA LIWE…ISHU NZIMA IKO HIVI…

admin February 5, 2023 7:04 am

Mlinda Lango chaguo la Pili wa Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Yanga  Abutwaleeb Mshery, anatarajiwa kwenda nchini Tunisia kwa ajili ya matibabu.

Mlinda Lango huyo kwa muda mrefu amekua nje ya kikosi cha Yanga akiuguza majeraha ya goti, ambayo yalipelekea klabu hiyo kumsajili kwa mkopo Metacha Mnata kupitia Dirisha Dogo.

Taarifa zinaeleza kuwa Msheri ataongoza na kikosi cha Yanga kuelekea Tunis-Tunisia kwa ajili ya mchezo wa Mzunguuko wa Kwanza Hatua ya Makundi Kombe la Shirikisho Barani Afrika, lakini atabaki huko kwa ajili ya kufanyiwa matibabu.

Msheri atapelekwa kwenye Hospitali iliyowatibu Kibwana Shomary na Yacouba Songne ambapo Matibabu waliyoyapata kwenye Hospitali hiyo inayosifika kwa kutoa tiba nzuri iliwasaidia kurejea Uwanjani mapema.

Kikosi cha Young Africans kinatarajiwa kuondoka jijini Dar es salaam Jumanne (Februari 07), tayari kwa mchezo wa Kundi D, Kombe la Shirikisho Barani Afrika utakaowakutanaisha dhdi ya US Monastir, Jumapili (Februari 12).

KUHUSU MAMBO YA CAF…MANGUNGU ATULIZA PRESHA SIMBA…AFICHUA MGOGORO NA M-BET… BAADA YA KUONA SIMBA YA MBRAZILI INAVYOCHEZA…MO DEWJI ASHINDWA KUJIZUIA…ACHUKUA MAAMUZI HAYA MAPYA…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply