Habari za Simba SC
Habari za michezo

HUU HAPA UKWELI KUHUSU HALI YA SIMBA GUINEA NA WALIVYOPOKELEWA UWANJA WA NDEGE..

admin February 11, 2023 7:24 am

Meneja Habari na Mawasiliano wa Klabu ya Simba, Ahmed Ally amesema kikosi hicho kimewasili salama nchini Guinea juzi saa 11 jioni na kila kitu kinakwenda sawa kuelekea mchezo wa kwanza wa hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Horoya.

Ahmed amesema hali ya hewa ya Mji wa Conakry ambapo mchezo wetu utafanyika ni sawa na jijini Dar es Salaam hivyo wachezaji hawatapata changamoto yoyote inayohusiana na hali ya hewa.

Ahmed ameongeza kuwa kikosi kimefanya mazoezi ya mwisho jana jioni katika uwanja wa (Stade General Lansana Conte)ambao utatumika kwenye mchezo wa leo.

“Tunamshukuru Mwenyezi Mungu tumefika salama nchini Guinea juzi jioni. Wachezaji walipewa mapumziko na wamefanya mazoezi ya mwisho jana jioni kabla ya leo kushuka uwanjani.

“Kwa kweli hatukupata changamoto yoyote ya nje ya uwanja, baada ya kufika usafiri ulikuwepo tayari kutupeleka hadi hotelini tulipofikia kwa hiyo hali ni nzuri,” amesema Ahmed.

MBRAZILI SIMBA AGOMA KUPAKI BASI ….YANGA WAVAMIA UWANJA WA WAARABU USIKU USIKU… KUELEKEA MECHI YA LEO…SAKHO AJIPA KIAPO KIPYA SIMBA..AFICHUA YA SAIDO NTIBAZONKIZA..

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply