Kiungo mshambuliaji wa Simba, Pape Sakho ameweka wazi kuwa lengo letu ni kuhakikisha tunashinda ugenini dhidi ya Horoya katika mchezo wa kwanza wa hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika utakaopigiwa leo Jumamosi.
Sakho amesema kila mchezaji anajua umuhimu wa mchezo huo na yupo tayari kuhakikisha anapigania timu kupata matokeo mazuri ugenini.
Akizungumzia kukosekana kwa kiungo mshambuliaji, Saido Ntibazonkiza amesema alitamani angekuwepo kikosini kutokana na ubora na uzoefu wake lakini siku zote majeruhi sio kitu kizuri kwa mchezaji.
“Maandalizi yetu ni mazuri, malengo yetu ni kushinda ugenini tutapambana ili kufanikisha hilo.
“Tunajua haitakuwa mechi rahisi, tutakuwa ugenini lakini tupo tayari kwa mpambano na mashabiki wetu tunawaomba mtuombee ili tukatimize malengo,” amesema Sakho.
Simba watashuka dimbani leo kukipiga na mabingwa wa Guinea, klabu ya Horoya katika mchezo wa pili wa kundi hilo ambalo linaongozwa na Raja Casablanca ya Morocco baada ya jana kuibuka na ushinidi wa goli 5-0 dhidi ya Vipers.