Home Habari za michezo BAADA YA KUZIONGOZA SIMBA NA YANGA…SENZO KUPEWA UBOSI WA LIGI KUU…

BAADA YA KUZIONGOZA SIMBA NA YANGA…SENZO KUPEWA UBOSI WA LIGI KUU…

Habari za Yanga

Ligi kuu nchini Botswana (BFL) huwenda ikamtangaza, Senzo Mbatha kuwa Mtendaji Mkuu baada ya Solomon Ramochotlhwane kujiuzulu nafasi hiyo miezi mitatu iliyopita.

Mbatha ambaye ni raia wa Afrika Kusini amewahi kuhudumu nafasi hiyo kwenye Klabu pendwa nchini za Simba SC na Young Africans kabla ya kuondoka kwake Tanzania.

Mwenyekiti wa BFL, Nicholas Zackhem Oktoba 9,2022 aliwahi kusema kuwa Rais wa Chama cha Soka nchini Botswana (BFA) Maclean Letshwiti alipendekeza jina la Senzo Mbatha ambaye CV yake inaonyesha ana uzoefu mkubwa na mchezo wa mpira wa miguu.

Kwa timu zetu zote alizozifanyia kazi, alileta mabadiliko ya katika uendeshaji na usimamizi wa soka hasa klabu kunufaika na mfumo wa kidigital katika nyanja tofauti.

Uwezo huo wa Senzo katika utawala sio jambo ambalo lilimjia ghafla bali alijiandaa na aliandaliwa kuwa na ubora na uwezo huo.

Alishawahi kufanya kazi katika klabu ya Orlando Pirates lakini pia aliwahi kuwa miongoni mwa wajumbe wa kamati ya maandalizi ya Fainali za Kombe la Dunia zilizofanyika 2010 huko Afrika Kusini.

SOMA NA HII  UJIO WA MANULA WAMPA WASIWASI MWARABU WA SIMBA