Home Habari za michezo BAADA YA SAWADOGO KUYUMBA MECHI NA WAMOROCCO…MBRAZILI SIMBA ASHUSHA PUMZI NA UJIO...

BAADA YA SAWADOGO KUYUMBA MECHI NA WAMOROCCO…MBRAZILI SIMBA ASHUSHA PUMZI NA UJIO WA KANOUTE…

Habari za Simba

Kocha Mkuu wa Simba SC, Roberto Oliviera ‘Robertinho’ amesema anayo furaha kuona kiuongo wake mkabaji anakuwa sehemu ya kikosi kitakachowavaa Azam FC kesho Februari 21, 2023 baada ya kumkosa kwenye mchezo wao uliopita wa Kimataifa dhidi ya Raja Casablanca akitumikia adhabu ya kadi tatu za njano.

Robertinho amesema, alimkosa nyota huyo kwenye mchezo huo muhimu ambao alipoteza kwa goli 3-0 lakini sasa anakwenda kumtumia kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya NBC ambayo anaamini itakuwa na ‘aproch’ tofauti.

“Ni furaha kwangu kumuona anarejea baada ya kukosa mchezo uliopita, anakwenda kuniongezea wigo mpana wa kufanya uchaguzi wa mtu wa kucheza kwani wanakuwa sasa wachezi wawili au watatu kwenye nafasi yake,” alisema Robertinho.

Simba SC wanawakaribisha Azam FC kesho kwenye dimba la Benjamini Mkapa wakiwa nafasi pili kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya NBC na pointi zao 53 huku Azam wao wakiwa nafasi ya nne na pointi zao 43.

SOMA NA HII  PAMOJA NA SIMBA KUSHINDA JUZI...RAGE ASHINDWA KUJIZUIA KWA YANAYOENDELEA..ATUPA DONGO ZITO ...