Home CAF CAF WAZIRUDISHIA ‘VIBE’ SIMBA NA YANGA…VIZUIZI VYOTE VYAFUTWA RASMI…

CAF WAZIRUDISHIA ‘VIBE’ SIMBA NA YANGA…VIZUIZI VYOTE VYAFUTWA RASMI…

CAF

Wakati Michauno ya Ligi ya Mabingwa na Kombe la Shirikisho Barani Afrika Hatua ya Makundi ikitarajiwa kuanza mwishoni mwa juma hili, Shirikisho la Soka Barani humo ‘CAF’, limetoa taarifa rasmi ikiyaagiza Mashirikisho ya soka ya nchi wanachama kuruhusu mashabiki kuingia viwanjani bila vizuizi.

Kwa zaidi ya misimu miwili ‘CAF’ ilikua inazuia idadi kubwa ya Mashabiki wa Soka kuingia viwanjani kushuhudia Michezo ya Michuano ya Ligi ya Mabingwa na Kombe la Shirikisho Barani Afrika Hatua ya Makundi, Robo Fainali, Nusu Fainali na Fainali kwa kuhofia maambukizi ya Ugonjwa wa Uviko-19.

‘CAF’ imetoa taarifa hiyo jana Jumatatu (Februari 06) ambayo imesambazwa kwenye Klabu zote shiriki, kupitia Mashirikisho ya soka ya nchi zao.

Aidha taarifa hiyo imeeleza mambo mbalimbali huku ikithibitisha kupungua kwa kasi ya maambukizi ya Uviko-19, hivyo Klabu shirikisho zinaweza kuingiza idadi kamili ya mashabiki Katika Viwanja vyao.

Klabu zinazoshiriki Ligi ya Mabingwa Barani Afrika Hatua ya Makundi msimu huu ni Al Ahly (Misri), Wydad AC (Morocco), Espérance de Tunis (Tunisia), Raja Casablanca (Morocco), Mamelodi Sundowns (Afrika Kusini), Zamalek (Misri), Petro de Luanda (Angola) na Horoya AC (Guinea).

Nyingine ni Simba SC (Tanzania), CR Belouizdad (Algeria), JS Kabylie (Algeria, Al Hilal (Sudan), AS Vita Club (DR Congo), Coton Sport (Cameroon), Al Merrikh (Sudan) na Vipers SC (Uganda).

SOMA NA HII  MUONEKANO WA UKURASA WA MBELE GAZETI LA SPOTI XTRA JUMANNE