Home Habari za michezo HUU NDIO UKWELI…..ILI SIMBA WATOBOE CAF HAKUNA ZAIDI YA HILI…WAKISHINDWA ‘WAKALIME’…

HUU NDIO UKWELI…..ILI SIMBA WATOBOE CAF HAKUNA ZAIDI YA HILI…WAKISHINDWA ‘WAKALIME’…

Habari za Simba

Hakuna namna! Ndivyo wadau wa soka na nyota wa zamani wa timu ya Simba wametamka baada ya kipigo cha timu yao cha mabao 3-0 dhidi ya Raja Casablanca juzi usiku katika mchezo wa pili wa makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika na kushauri timu hiyo sasa ipambanie nafasi ya pili ili kusonga mbele.

Wamekwenda mbali zaidi na kusisitiza kwamba, Simba inapaswa kupambania pointi tisa wakianza na ijayo ya ugenini Uganda dhidi ya Vipers Jumamosi hii, kisha kuja kuikaribisha Vipers jijini Dar es Salaam na kuwasubiri pia nyumbani Horoya ya Guinea kabla ya kumaliza hatua ya makundi ugenini dhidi ya Raja.

“Kinyume cha hapo nafasi yake kusonga mbele itakuwa ni ngumu, hizi pointi tisa ndizo zitaibeba, hakuna namna nyingine zaidi ya kuhakikisha wanapigania kumaliza kwenye nafasi ya pili katika kundi lake,” alisema mkurugenzi wa maendeleo ya michezo nchini, Ally Mayay.

Katika kundi C, Simba imecheza mechi mbili na kupoteza zote, ilichapwa na Horoya ugenini bao 1-0 kisha juzi ikaruhusu kipigo cha mabao 3-0 nyumbani kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.

Japo kocha, Roberto Oliveira ‘Robertinho’, amekiri walishindwa kutumia vizuri nafasi za kufunga, nyota wa zamani na wadau wa soka wamemshauri kubadili mfumo wa uchezaji kwenye kikosi chake.

“Hii ya kumiliki tu mipira bila faida haina maana tena, kwenye mechi zijazo wachezaji wafanye kama Sakho (Pape) inaweza kuwasaidia.

“Kwa kuwa kushinda ugenini kule Morocco kwenye marudiano na Raja Casablanca hakuna dalili hizo na Raja wanaonekana ndiyo wataongoza kundi hilo, Simba haina namna nyingine zaidi ya kupambani nafasi ya pili kwa kutafuta pointi tisa kwa Vipers ugenini na nyumbani na Horoya nyumbani,” alisema Mayay.

Hata hivyo, kocha Robertinho amesisitiza bado wana nafasi ya kufanya vizuri kwernye michezo minne iliyosalia ya makundi akiamini timu yao ilicheza vizuri juzi japo hawakuwa wanafika ndani ya boksi la wapinzani wake mara kwa mara.

“Tulicheza mpira mzuri lakini hatukuwa tunashambulia sana ndani ya boksi, kuna muda ukipata nafasi ndani ya boksi inabidi uifanyie kazi, unajua huku kwenye hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa hakuna timu ndogo.”

Nyota na kocha wa zamani wa timu hiyo, Abdallah Kibadeni alisema timu hiyo inapaswa kucheza kete zake vema.

“Ukifanya hesabu ya matokeo ya jana na Raja na yale ya awali na Horoya na mechi nne zilizobaki, Simba ili iwe salama lazima ishinde tatu na si vinginevyo, mechi ya jana (juzi) tumeona timu yetu ilizidiwa,” alisema Kibadeni.

Kipa wa zamani wa timu hiyo, Mosses Mkandawile alisema kocha anapaswa kuongeza mazoezi kwenye eneo la beki akitolea mfano mabao waliyofungwa juzi.

“Onyango na Inonga wanapaswa kuongeza mazoezi, mfano bao la kwanza watu wanapiga pasi hakuna aliyewakaba hadi wanafunga, la pili walimshau mtu,” alisema.

SOMA NA HII  VIINGILIO VYA IHEFU vs YANGA HIVI HAPA