Home Habari za michezo BAADA YA YANGA KUIHARIBIA SIMBA MSIMU HUU…SENZO AIBUKA NA HILI…ATUMA ‘KOMBORA JIPYA’...

BAADA YA YANGA KUIHARIBIA SIMBA MSIMU HUU…SENZO AIBUKA NA HILI…ATUMA ‘KOMBORA JIPYA’ MSIMBAZI….


YANGA imeondoka kibabe jijini Mwanza baada ya kuichapa Simba kwa bao 1-0, lakini bosi wao mmoja wa zamani ametuma salamu za uchokozi zitawaumiza zaidi wenzao wakati msimu ukielekea ukingoni kwa sasa.

Mtendaji Mkuu wa Yanga, Senzo Mazingiza amesema kuwa umekuwa msimu mtamu baada ya kufanikiwa kuwavua taji, Simba kwa kuichapa ndani ya dakika 90 msimu huu.

Yanga iliichapa Simba kwa bao 1-0 lililowekwa kimiani na kiungo mshambuliaji, Feisal Salum ‘Fei Toto’ dakika ya 26 katika mechi ya nusu fainali ya michuano ya Kombe la Shirikisho (ASFC), uliopigwa kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, jijini Mwanza.

Senzo, aliyewahi kuwa Mtendaji Mkuu Simba alisema baada ya kuwakosa mara mbili katika Ligi Kuu Bara mechi zote zikiisha kwa suluhu sasa wanaenda kulisaka taji la pili la ASFC kupitia mgongo wa Simba.

“Soka la Tanzania unataka vitu vya namna hii mashabiki wetu walikuwa kila wakati wanaumia wakituambia wanatamani kuona tunawafunga Simba, angalau mechi moja kisha tuchukue ubingwa,” alisema Senzo na kuongeza;

“Hapa nadhani sasa watafurahia kama ambavyo uongozi tunafurahia na wadhamini wetu wote,huu ushindi unaleta nguvu kwetu tukichukua mataji mbele ya ushindi kwao,hapa sasa ubingwa unakuwa mtamu.

Aidha Senzo alisema Yanga haijamaliza kazi watashuka na nguvu kubwa kwa yoyote watakayekutana naye fainali katika mchezo .

Alisema kikosi chao kimedhihirisha kina nguvu ya kushinda mechi kubwa na ndogo na kwamba hawataidharau timu yoyote kati ya hizo ili wachukue taji hilo.

“Tunaishi katika malengo yetu,tulijipanga kuhakikisha tunashinda hii mechi dhidi ya Simba lakini sasa tumetinga fainali huko sasa tutaingia kwa nguvu zaidi bila kuangalia tunakutana na nani,hii ni fainali lazima iwe na ugumu wake na sio kudharau.

“Tuna wachezaji bora na benchi bora la ufundi chini ya Kocha Nabi (Nasreddine) tutawasikiliza wanachotaka na uongozi tutayafanyia kazi tunalitaka hili komb la pili pia.”

SOMA NA HII  LOMALISA ASHTUA YANGA...AFUNGUKA A-Z MPANGO WA SIRI WA YEYE KUTUA JANGWANI....